HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 26, 2024

MASHINDANO YA RIADHA AFRIKA MASHARIKI (EAAR), U 20&18 YAANZA KUTIMUA VUMBI AMAAN COMPLEX ZANZIBAR

NCHI saba zimejitokeza kuchuana katika Mashindano ya Vijana chini ya Miaka 20 na 18 ya Riadha Afrika Mashariki (EAAR), kwenye Uwanja wa Amaan Complex visiwani Zanzibar.


Mashindano hayo yatafanyika kwa siku mbili, Aprili 26 na 27.
Katika siku ya kwanza, Aprili 26, mchuano umeonekana mkali humu Kenya ikionyesha kung'ara huku Uganda, Tanzania Bara, Djibouti, Zanzibar, Sudan Kusini na Somalia zikifuatia.


Mashindano hayo pia yamehudhuriwa na viongozi wa EAAR wakiongozwa na Mwenyekiti Luteni Jenerali mstaafu Jackson Tuwei kutoka Kenya, Katibu Mhandisi Sidique Ibrahim kutoka Sudan, Rais wa Riadha Tanzania (RT), Silas Isangi,  Makamu wake William Kallaghe, Kaimu Katibu, Wakili Jackson Ndaweka na viongozi wengine kutoka nchi shiriki wakiongozwa na wenyeji Zanzibar chini ya Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Zanzibar, Makame Ali Machano.



No comments:

Post a Comment

Pages