RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho
Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo
anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda
ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu
ambako atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya
ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19,
2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA
WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, AGOSTI 18, 2016.
No comments:
Post a Comment