HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 15, 2016

ZADIA inatoa mkono wa pole kwa Wazanzibari wote Kufuatia kifo cha Mzee Aboud Jumbe

215 459 4449
zadia.org

انا لله وانا اليه راجعون

Jumuiya ya Wazanzibari Nchini Marekani (ZADIA), imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
Mzee Jumbe aliyewahi kuwa rais wa Zanzibar na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika harakati za kuleta maendeleo na mabadiliko ya kisiasa visiwani Zanzibar.
Chini ya Uongozi wake, kwa mara ya kwanza Zanzibar ilipata katiba yake na hivyo kuanzishwa kwa Baraza la Wawakilishi kama chombo cha uwakilishi wa Umma na kutunga sheria.
Atakumbukwa pia kwa msimamo wake shupavu wa kupigania haki sawa ndani ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar khususan madai yake ya kutaka kuwa na serikali tatu.
Marehemu Jumbe alikuwa rais wa Zanzibar kuanzia mwaka 1972 kufuatia kifo cha rais wa kwanza wa Zanzinbar Marehemu Abeid Aman Karume. Alilzaimishwa kujiuzulu nyadhifa zake zote za kisiasa mwaka 1984 baada ya kutuhumiwa kuchafua hali ya hewa ya kisisasa Zanzibar. 

Uchafuzi ambao si chochote ila ushupavu wake wa kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mnasaba huu, ZADIA inatoa mkono wa pole kwa Wazanzibari wote kwa ujumla kwa kuondokewa na kiongozi wao mzalendo. 
Aidha kono wa pole makhasusi uwafikie wanafamilia ya Marehemu, tukimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba, na kumwomba Mola Mlezi amlaze marehemu mahali pema Peponi. Amin.
Omar H Ali, Mwenyekiti, ZADIA
Agosti 14, 2016

No comments:

Post a Comment

Pages