HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 15, 2016

NETBALL TANAZANIA YAJITANGAZIA UBINGWA BAADA YA KUIFUNGA KENYA

Na Selemani Semunyu, JWTZ
 
Timu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kwa Mpira wa Pete wametangaza ubingwa wa michuano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki kwa mchezo huo yanayoendelea katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda.
 
Tanzani]a ilifikia hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Kenya  39-33 katika Mchezo uliokuwa vuta nikuvute ikiwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Timu hiyo kushinda na hivyo kupata alama ambazo haziwezi kufikia na Timu yeyote. 
 
Katika Mchezo huo Tanzania ilianza vyema tangu Robo ya Kwanza ambapo ilitoka 17-13 wakati robo ya pili 20-16 huku robo ya Tatu wakitoka 31 kwa 24 na mwisho Tanzania kuibuka Washindi.
 
Nahodha wa Tanzania Dorita Mbunda alisema wanafuraha kwa kurejesha ubingwa walioupoteza mwaka jana na kuchukuliwa na Uganda.
 
Nahodha wa Uganda Carlo Alepo alisema walikuwa na wachezaji wachanga amabao ni wageni katika mashindano hivyo wanajiandaa kwa michuano ijayo kwani wachezaji wao watakuwa na uzoefu Tayari wa Mashindano.
 
Kikosi cha Tanzania kilichoibuka na Ushindi huo  ambacho kilicheza Mwanzol had Mwisho wa mchezo huo ni  Dorita Mbunda,Faraja Malaki,Joyce Kaira,Veronica Patric,Mwanaidi Hassan,Nasra Suleiman Na Lulu Joseph.
 
Kwa upande wake  MaKocha wa Timu hiyo Grace Mgyabuso na Argentina  Kienzevya kwa Nyakati tofauti walisema  ahadi waliyoitoa kwa Watanzania na Mkuu wa majeshi wameitimiza kilichobaki ni kusubiri kukabidhiwa kombe. 
 
Naye Kanali  Mary Hiki wa Tanzania  aliwapongeza wachezaji na kuwashukuru Watanzania kwa maombi yao yaliyowawezesha kuibuka na ushindi huo ambao aliuita ni muhimu kwa Taifa. 
 
Awali Timu ya Tanzania iliifunga Timu ya Rwanda ambayo ni mabingwa wattezi kabla ya Kuwafunga Wenyeji Rwanda kwa matokeo ambayo hayajafikiwa na Timu yeyote katika Michuano hii.

No comments:

Post a Comment

Pages