Na Bryceson Nyeregete, Kisasa-Dodoma
BAADA ya Miaka takribani 28 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma kutokuwa na Makazi rasmi ya Askofu, Hatimaye Uongozi uliopo kwa kuwashirikisha Wakristo, umefanikiwa kuanza Ujenzi wa Makazi hayo utakaogharimu Milioni 300/-, na inatarajiwa ikamilike kati ya Miezi Sita hadi Mwaka mmoja.
Akizungumzia Mafanikio hayo alipohojiwa na Gazeti la Upendo hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Robert Mgaya, alianza kwa kuwashukuru Wakristo wote wanaoendelea kuchangia Ujenzi huo ambao sasa umefikia kwenye Lenta, kutokana na Mchango wao wa Fedha,Vifaa na Nguvu zao.
Mbali ya kuwashukuru Wakristo, Mgaya pia ameishukuru Kamati ya Maono ya Ujenzi wa Makazi hayo inayoratibiwa na Mwenyekiti, William Lema, sambamba na Mkuu wa Miradi wa Dayosisi ya Dodoma, Mchungaji Eliwasiri Mbwambo, na Wachungaji wa Dayosisi hiyo kwa ushirikiano wao.
Mwenyekiti wa Ujenzi [Lema] alisema, Nyumba hiyo inayojengwa eneo la Kisasa ina Vyumba Vinne (4), Wiwili (2) vya ‘Master Bedroom’ (Self Contained), Viwili vya kawaida, Maktaba Ndogo ya kusomea (Mini-Library), Jiko, Chumba cha Kulia Chakula (Dining), Sebule (Seating room), Choo na Bafu ya Jumuia (Public), na Nyumba Ndogo ya Walinzi (Servant Quarter).
Lema alisema, Jumanne Septemba 6, mwaka huu wanatajia kufunga Lenta, ambapo naye amewashukuru sana na kuwapongeza Wakristo na Watumishi wote kwa Ukarimu wao kwa Mungu wanayemtumikia kwa Mali zao huku akisema anaamini atawarudia Baraka nyingi za mwilini na za rohoni.
“Japo Kiganja chetu tunatumia kumchotea Mungu kitaonekana kidogo, lakini Kiganja cha Mungu atakachotuchotea yeye (Mungu) na kutupatia sisi (Baraka zake), ni Kujaa, Kushindiliwa, Kusukwasukwa hata kumwagika.
”Kama Nyuki wanavyoingia na Kutoka katika Mzingi toka mawaindoni wakiwa Asali toka kwenye Maua, basi vivyo hivyo nawatakia Baraka za Mungu wakristo wote katisha Shughuli zao za Mikono, Biashara, Mashamba, sehemu za Kazi, na popote katika kufanikisha ujenzi huo” alisema Lema akinukuu andiko la Kitabu cha Luka 6:38.
Naye Mchungaji wa Miradi wa Dayosisi Mbwambo alikiri Ujenzi huo kwenda katika hatua nzuri, ambapo licha ya kusema wanatarajia kufunga Lenta wiki hiyo, aligusia kuwa Serikali inahamia Dodoma, hivyo kuna haja kubwa ya kuitazama Shule ya Kidato cha Sita iliyokusudiwa eneo la Chuo cha Mipango Dodoma ili ifanyiwe Kazi maana KKKT ina Waumini wengi ambao ni Walimu, kwa hiyo anakaribisha Ushauri wao!.
Aidha Baba Askofu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Amoni Kinyunyu, alisema“Huu ndio wakati ambao Mungu alitaka tujenge Makazi hayo ya Askofu, kama ambavyo tangu enzi ya Wafalme na Manabii huko Nyuma, walijenga Nyumba ya Bwana katika maeneo kadhaa baada ya wengi kutangulia, akisema utanijenga Madhabahu na kadhari”.alisema Kinyunyu akiwashukuru Wakristo na Watumishi wote wa KKKT Dodoma.
No comments:
Post a Comment