Basi walilokuwa wanasafiriamashabiki wa timu ya Simba baada ya kupata ajali katika eneo la Mkambala katikati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi,
ametuma salamu za rambi rambi kwa Rais wa klabu ya Simba SC Bw. Evans Aveva kufuatia
vifo vya mashabiki wa klabu hiyo, viliyotokea jana katika ajali ya barabarani
eneo la Makunganya mkoani Morogoro.
Katika salamu zake Rais Malinzi amesema, TFF imezipokea kwa
masikitiko taarifa hizo za ajali na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu
nchini, wanawapa pole wafiwa wote na mwenyezi Mungu awape nguvu majeruhi waweze
kupata nafuu na kupona kwa uharaka zaidi.
Aidha Rais Malinzi ameagiza
michezo yote ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania itakayochezwa wikiendi hii nchini, kusimama kwa dakika moja
ili kuwakumbuka mashabiki waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
MALINZI AKUTANA NA
MAKAMU WA RAIS WA FIFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF jana ijumaa ilipokea ugeni
wa makamu wa Rais wa FIFA ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu
nchini Jordan, HRH Prince Ali Bin Al Hussein. (picha ya Rais Jamal Malinzi na
HRH Ali imeambatanishwa)
Jioni Prince Ali Bin AliHussein na ujumbe wake walifanya
mazungumzo na Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi katika hoteli ya Kilimanjaro Kempsinki
(Hyatt) iliyopo jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo, zaidi waligusia maeneo kadhaa ya
ushirikiano kati ya TFF na Chama cha Mpirwa wa Miguu nchini Jordan (JFA), hasa
katika maeneo ya maendeleo ya mpira wa vijana, makocha na waamuzi.
HRH Prince Ali Bin Al Hussein ambaye ni mgombea wa nafasi ya urais
FIFA mwaka huu, ameondoka leo mchana kurudi nyumbani kwake Jordan.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment