Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba (katikati), akizungumza na madereva 10 wa Tanzania waliotekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni waasi Jamhuri ya Demokrasia ya Conco (DRC), wakati wa hafla fupi ya kuwapokea iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Kulia ni Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba na kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Afrika katika wizara hiyo, Balozi Samweli Shelukindo.
Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Mmiliki wa Kampuni ya Simba Logistic ambayo magari yake na madereva walitekwa, Azim Dewj (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ya kuwapokea madereva hao.
Dereva Mbwana Said (kulia), akielezea jinsi walivyotekwa.
Picha ya pamoja na viongozi waliowapokea.
Na Dotto Mwaibale
MADEREVA 10 wa Tanzania waliotekwa na watu wanaodhaniwa ni waasi Jamhuri ya Demokraia ya Congo (DRC) wamesema waliponea tundu la sindano kuuawa.
Kauli hiyo imetolewa na madereva hao katika hafla ya kuwapokelewa iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo jioni.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mbwana Said alisema analishukuru jeshi la Congo kwa jitihada kubwa walioifanya kwa ajili ya kuokoa maisha yao."
" Tunaishukuru serikali ya Congo kwa kutuokoa kwani tulikuwa katika wakati mgumu na leo kuungana tena na ndugu zetu" alisema Said.
Alisema walilazimia kutembea kwa muda mrefu huku risasi zikirindima kati ya majeshi ya serikali na waasi hao hadi walipofanikiwa kutuokowa kutoka kwenye mikono ya waasi hao.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba aliishukuru serikali ya Congo kwa jitihada iliyoifanya na kufanikiwa kuwaokoa madereva hao.
Balozi wa Congo nchini Jean Mutamba aliwataka madereva hao kuacha viza na nyaraka zao ubalozini pindi wanapo safiri na kurudi ili iwe rahisi kuwatambua pale wanapopata matatizo.
"Tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya na kutoa wito kuwa waendelee kusafiri kwa kufuata taratibu zilizopo," alisema Mutamba.
No comments:
Post a Comment