HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2016

MH. SUBIRA MNGALU AKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA AJILI YA UJENZI WA VYOO CHUO CHA MAENDELEO KISARAWE

01
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikabidhi mifuko ya saruji na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa vyoo kwa Bw.Herry Mjengelaungu Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Kisarawe katika hafla iliyofanyika chuoni hapo leo kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kisarawe Bw. Mtera Mwampamba na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi. Happiness Saneda.
1
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akizungumza na wakufunzi na wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Kisarawe kabla ya kukabidhi vifaa katika chuo hicho kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Happiness Saneda.
02
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akipiga picha na mkuu wa chuo hicho pamoja na wakufunzi mara baada ya makabidhiano.
3
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikagua chumba cha kompyuta.
4
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo angalia.
5
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikagua mabweni ya chuo hicho kutoka kwa mkuu wa chuo Bw. Herry Mjengelaungu.
...................................................................................

NA MWANDISHI WETU

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu(CCM) ametoa msaada wa vifaa za ujenzi wa vyenye thamani ya sh. milioni moja kwa Chuo Maendeleo ya Wananchi(FDC) Kata ya Kazimzumbwi, Kisarawe mkoani Pwani. Subira alimkabidhi msaada wa vifaa hivyo ambavyo ni saruji,mchanga,mbao, matofali, nondo na kokoto kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa choo cha wavulana baada ya cha awali kubomoka na wanafunzi kulazimika kutumia choo kimoja cha wasichana.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo jana, Subira alisema anaamini ujenzi wa choo hicho utakamilika mapema kwa kuwa unafanywa na nguvu kazi ya vijana wenyewe chini ya usimamizi wa wakufunzi wao. Mbunge huyo alisema kwamba anatambua kwamba ana wajibu wa kuhakikisha afya za vijana wanaosoma chuoni hapo zinakuwa salama hivyo ametoa kama kiongozi na mzazi wa watoto hao.

Alisema aliguswa baada ya kutembelea chuo hicho mwezi mmoja uliopita na kuona changamoto nyingi zinazowakabili wanafunzi na watumishi wa chuo hicho ambapo alihidi kusaidia na kuhamasisha viongozi wengine wafike chuoni hapo. 

Subira alisema vyuo hivyo na vyuo vya ufundi vilivyopo chini ya VETA ni muhimu hususan wakati huu ambao nchi inaelekea kwenye uchumi wa viwanda,vyuo hivyo ndivyo vitakavyozalisha wataalamu watakaofanya kazi kwenye viwanda. 

Alisema vyuo hivyo ambavyo kwa Mkoa wa Pwani vipo Kibaha, Kisarawe na Ikwiriri wilayani Rufiji, miundombinu yake ni chakavu na wanakabiliwa na changamoto nyingi hivyo wakati serikali inaangalia namna, viongozi na wadau wanapaswa kusaidia. 

Mbunge huyo alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happines Senada na uongozi wa halmashauri kuwatumia vijana wa chuo hicho kuwapa kazi hususan za ujenzi wa vyoo vya shule za msingi ili kusadia vyuo hivyo na kwamba sheria ya manunuzi imeruhusu kutumia makundi maalumu ya vijana na wanawake.

Awali akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho Mkuu wa Wilaya, Happines alisema chuo hicho kina umuhimu mkubwa hivyo atahakikisha changamoto zinazowakabili zinatatuliwa kwa kushirikiana na wadau. 

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Heri Mjengelaungu, alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu chakavu, tatizo la maji, umeme, vifaa vua kufundishia kwa vitendo , haina magari.

Alimshukuru mbunge huyo kwa msaada wake wa vifaa vya ujenzi wa choo hicho kwa kuwa hali ni mbaya hivyo watahakikisha kwa kushirikiana na wanafunzi na wakufunzi choo hicho kinakamilika mapema zaidi kwa kuwa shimo limeshachimbwa.

No comments:

Post a Comment

Pages