Na Bryceson Mathias, Mvomero
MTUHUMIWA, Ally Rashid, wa Kunke Mvomero, aliyedaiwa kutaka kumchinja mwanawe, Juma Ally, kwa kosa la kupoteza Mbuzi wawili na kukimbilia kwa Sangoma ili asitiwe hatiani na mkono wa sheria,hatimaye amekamatwa na atafikishwa mahakamani Septemba 11, mwaka huu kujibu shitaka hilo.
Akithibitisha kukamatwa kwa Rashid, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mashariki, Kijiji cha Kunke Kata ya Mtibwa wilayani Mvomero, Rashid Issa, amethibitisha kukamatwa kwa Rashid mara aliponusa tu nyumbani kwake, baada ya wasamaria wema kijiji hapo kutoa taarifa.
Aidha wananchi waliotaka wasitajwe maji yao waliokuwa wakimgoja kwa hamu kama mpira wa Kona walidai, Ally alikimbilia porini kwa Sangoma ili amgange jambo hilo lisahaulike asikamatwe, lakini cha ajabu dawa za Sangoma hazikufua dafu na mara aliporejea tu nyumbani alikamatwa.
Jeshi la Polisi Kituo cha Mtibwa ambapo viongozi wake wamedai siyo wasemaji wamethibitisha kumkamata Rashid, Jumatatu Septemba 5, na kusema, atafikishwa kizimbani Mahakama ya Mwanzo Mtibwa ili kujibu shitaka la kukusudia kuua.
Hata hivyo baada ya kulala rmahabusu kwa siku mbili, Rashid amefanikiwa kuwekewa dhamana na siku zake, hivyo kungojea siku ya shitaka hilo litakaposomwa kwa mara ya kwanza, huku wakazi wa Vijiji vya Kunke, Kidudwe na Mtibwa wakitarajia kuhudhuria kwa wingi kutoakana na ksi hiyo kuvuta hisia za wengi, wakishangaa Baba kutaka kumchinja mtoto kwa kupoteza Mbuzi.
Agosti 17, ,2016 saa 10 jioni, Ally alipigiwa simu na ndugu zake kuhusu kupotea kwa mbuzi hao, ambapo aliporudi nyumbani kwa hasira alimfuata mtoto huyo Kijiji jirani (Kidudwe) kwa Mama yake Mzazi alikokimbilia na kumrejesha Kunke.
Awali ilidaiwa, Rashid alipofika na Juma Nyumbani Kunke, alimhoji mbuzi amepotezea wapi! Na alipojibu kuwa haelewi alimfunga Kamba kwenye Miguu na Mikono na kutaka kumchinja, lakini kwa bahati nasibu dada yake aliyetambulika kwa jina la Mama Wawili, alipiga kelele na wananchi wakamuokoa, ingawa Rashid tayari alimjeruhi Mama huyo katika purukushani.
“Ally alipoona mambo ni makubwa alikimbilia na kutokomea mashambani baada ya kusikia ukiitaarifu Polisi kuhusiana na tukio la yeye kutakiwa kuwekwa nguvuni kwa kusa hilo la jina”.alisema Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mashariki Kijiji cha Kunke, Kata ya Mtibwa Mvomero Issa.
Mtoto Juma amekiri kupoteza mbuzi bila kukusudia, na kudai alikimbilia kwa mama yake Kidudwe akiogopa kuadhibiwa na baba yake, jambo ambalo wenyeji wamedai mtoto huyo aliachishwa shule achunge ng’ombe kutokana na wazazi hao kutengana kwa vile alikuwa na wake wawili.
Jeshi la Polisi mtibwa limekiri kupokea tuhuma ya mzazi huyo (Ally) kutaka kumchinja Mtoto wake na kutoroka, lakini hadi tunakwenda mitambuni tayari kulikuwa na taarifa za kukamatwa kwake kutokana na ushirikiano na wananchi ambao walikarisishwa na kitendo chake cha kutaka kumchinja mwanae.
No comments:
Post a Comment