HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 12, 2022

ABDULRAHMAN KINANA ASAIN KITABU CHA MAOMBOLEZO KUFUATIA KIFO CHA KOMRED DOS SANTOS

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Abdulrahman Kinana  amesaini kitabu cha maombolezo tarehe 12 Julai, 2022 katika Ubalozi wa Angola Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Komredi José Eduardo dos Santos, kilichotokea Ijumaa, Julai 8, 2022. nchini Hispania.

Ndg. Abdulrahman Kinana Ameongozana na Katibu Wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Abdulrahman Kinana  akisaini kitabu cha maombolezo tarehe 12 Julai, 2022 katika Ubalozi wa Angola Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Komredi José Eduardo dos Santos, kilichotokea Ijumaa, Julai 8, 2022. nchini Hispania. Pichani pamoja nae ni Katibu Wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka (aliyesimama Kwanza Kushoto) Pamoja na Balozi wa Angola Nchini Tanzania Mhe. Sandro De Oliveira. (katikati).
Balozi wa Angola Nchini Tanzania Mhe. Sandro De Oliveira akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Abdulrahman Kinana mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo tarehe 12 Julai, 2022 katika Ubalozi wa Angola Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Komredi José Eduardo dos Santos, kilichotokea Ijumaa, Julai 8, 2022.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Angola Nchini Tanzania Mhe. Sandro De Oliveira alipokwenda kusaini kitabu cha maombolezo tarehe 12 Julai, 2022 katika Ubalozi wa Angola Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Komredi José Eduardo dos Santos, kilichotokea Ijumaa, Julai 8, 2022. Picha: CCM Makao Makuu.
 

No comments:

Post a Comment

Pages