HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 30, 2016

NSSF YAWAFIKIA WAJASILIAMALI MBEYA

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeshiriki maonesho ya wajasiriamali (SIDO) yanayofanyika mkoani Mbeya.


Akizungumza Ofisa Masoko na Uhusiano, Anna Nguzo, alisema wajasiliamali wanaweza kufaidika na NSSF kupitia mpango wa Hiari Scheme. 

Alisema mpango huo ni mahususi ulioanzishwa kwa nia ya kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa watu walio katika sekta binafsi ambao wamejiajiri wenyewe.

"Mwanachama wa Hiari anaweza faidika na mafao yote yanayotolewa na NSSF ikiwemo Pensheni ya Ulemavu, Pensheni ya Urithi, Matibabu bure kwa mwanachama na familia yake inayojumuisha mke au mume na watoto wanne wasiozidi miaka 18 au 21 kama bado wanasoma,"alisema.

Pia alisema mwanachama anaweza kufaidika na mafao ya kuumia kazini pamoja na msaada wa mazishi.

Alisema katika maonesho hayo NSSF inatoa elimu kwa umma kuhusu hifadhi ya jamii na inaandikisha wanachama wapya pamoja na kupokea maoni mbalimbali.

Maonyesho hayo yanatarajiwa kufikia kilele Oktoba 3, mwaka huu ambapo yanafanyika katika viwanja vya City garden Sokoine jijini Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Pages