Naibu Katibu Mtendaji –Uchumi jumla kutoka Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete, akiwaonyesha maafisa mipango kutoka mikoa ya Arusha, Tanga, na Kilimanjaro mwongozo wa kusimamia uwekezaji wa miradi ya Umma.
Washikiri wa mafunzo ya Uwekezaji katika miradi ya umma wakifuatilia kwa makini mafunzo.
Na Oyuke Phostine
Wizara ya Fedha na Mipango – Tume ya Mipango inatoa mafunzo kwa maafisa mipango kutoka mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro ili kuwawezesha kuchambua na kuchagua miradi itakayoleta tija kwa taifa na inayoendana na Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Miaka Mitano.
Akizindua mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku tani katika kanda ya kaskazini jiijjini Arusha, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshuhghulika na Biashara za Kimataifa Bw. Paul Sangawe alibainisha kuwa lengo kuu la mafunzo haya limejikita katika kuimarisha uwezo wa maafisa mipango ili waweze kuibua miradi inayotekelezeka kwa urahisi na ufanisi.
Uwepo wa mwongozo huu katika uwekezaji wa miradi ya umma utasaidia kuboresha usimamizi na utekelezaji wa miradi ya umma kwa kuonyesha taratibu za kuzingatiwa ili kuhakikisha miradi iliyochaguliwa inaendana na bajeti ya maendeloa ya taifa.
“Baada ya mafunzo haya, ni mategemeo yetu kuwa mwongozo huu utawasaidia maafisa mipango kufanya upembuzi makini na uliyo sahihi ili kuja na miradi bora itakayotuepusha na matumizi mabaya ya fedha za umma saula ambalo kwa kipindi cha nyuma limekuwa likijitokeza huko nyuma. Hivyo jitihada hizi ni vema zikazaa matunda chanya” alisema Bw. Sangawe.
Kutokana na kutokuwepo kwa mwongozo wa kupembua na kuchagua miradi ya uwekezaji katika sekta ya umma Tume ya Mipango imeandaa Mwongozo kwa maafisa mipango wote nchini. Mwongozo huu utasadia kwa kuelekeza taratibu na kanuni zitakazotumika kataka kuchagua, kufadhili, kutekeleza na hata kuperemba na kutathimini miradi ya umma.
Ili kufikia malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, uchambuzi wa kitaalamu katika masuala ya fedha, athari za kiuchumi na kijamii katika miradi tajwa inapaswa kusimamiwa vema ili kuleta uwiano sawia kati ya miradi hiyo iliyochaguliwa na bajeti ya taifa ya miradi ya maendeleo.
“Lengo hilo linabeba matarajio ya wananchi wengi, japokuwa si suala ambalo ni rahisi kutekeleza bila kuwa na nidhamu katika uchaguzi wa miradi. Namana pekee ya kulifikia hii ndoto ni kwa kuhakikisha kidogo tulichonacho tunakitumia katika vipaumbele vya msingi vya taifa na inatumika ipasavyo” aliongeza Bw. Sangawe.
Mwongozo huu katika uwekezaji wa umma unakuwa ni muhimili mkubwa katika utelezaji wa miradi ya maendeleo iliyopendekezwa katika Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa ambao umelenga kutumia kiasi cha trilioni 11.8 kila mwaka ndani ya mwika mitano ijayo. Hivyo kiwango hiki kikubwa cha fedha ni lazima kifadhili miradi muhimu ya miundombinu na rasilimali watu.
No comments:
Post a Comment