HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 28, 2016

WATANZANIA WAASWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII


Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Msika akifafanua jambo wakati wa semina ya hifadhi ya Jamii kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Onorius Njoke. (Picha na Francis Dande) 
 Washiriki wa semina hiyo.
 Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Onorius Njoke akijibu maswali ya waandishi wa habari.


NA JANETH JOVIN

ZAIDI ya asilimia 90 ya watanzania bado awajiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii licha ya elimu inayozidi kutolewa na wadau mbalimbali  juu ya umuhimu wa mifuko hiyo.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Msika wakati wa semina ya siku moja kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na mamlaka hiyo.

Alisema mpaka sasa ni asilimia 8.8 sawa watu Milioni moja tu ndio waliojiunga na mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii nchini na kudai kuwa bado kunahitajika kutolewa elimu ya ziada ili jamii itambue umuhimu wa mifuko hiyo.

“Watu awajui  kuwa ukijiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kuna faida kubwa sana katika maisha yao hata katika nchi kwani mifuko hii inasaidia kupunguza umaskini na kuwa na taifa tegemezi,” alisema Msika.

Alisema suala la mifuko ya hifadhi ya jamii linamuhusu kila mtanzania bila kujali itikadi ya dini, vyama wala kabila hivyo ni muhimu kila mtu kujiunga kwani hakuna ajuaje kesho yake.

“Majanga yanaweza kumpata kila mtu na mifuko hii ya hifadhi ya jamii hipo kwaajili ya kutulinda pindi tunapopatwa na majanga hayo lakini wengi wao awajui umuhimu wake hivyo sisi kama wasimamizi wa mifuko hii tutaendelea kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi kujiunga na mifuko hiyo.

“Sisi kama SSRA tulianza kazi mwaka 2010 na wakati tunaingia idadi ya wanachama katika mifuko yote ya hifadhi ya jamii ilikuwa ni 900,000 lakini hivi sasa wapo zaidi ya milioni tumepiga hatua kidogo tunajivunia hilo lakini bado kunahitajika nguvu za ziada ili kuongeza idadi hiyo na kuliangalia hilo tumeanzisha mkakati wa kupanua wigo wa kuwapata wanachama,” alisema.

Aidha alisema ili kuongeza idadi ya wanachama katika mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii pia wameanzisha mkakati wa mawasiliano ambao unalenga kuangalia ni kwa namna gani wataweza kuwafikia walengwa na mifuko hiyo kwa haraka zaidi.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Sheria SSRA, Onorius Njole alisema ni kosa la jinai kwa mwajiri kumchagulia mwajiliwa wake mfuko wa hifadhi ya jamii hivyo amewataka wafanyakazi wote waliochaguliwa mifuko ya kujiunga walipoti taarifa hizo kwao na kwenye mamlaka husika.

“Ni kosa kubwa tena la jinai kwa mwajili kumchagulia mfanyakazi wake mfuko way eye kujiunga nawaomba watu wasikubali kufanyiwa hivyo na ikiwezekana waende kulalamika na kulipoti kwenye mamlaka husika,” alisema

No comments:

Post a Comment

Pages