Moja ya Ndege mpya ya serikali iliyokodishwa kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier Dash 8 Q400 ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha.
Moja
ya Ndege mpya ya serikali iliyokodishwa kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier Dash 8 Q400 ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha
wakati maafisa wa Mamlaka ya Anga(TCAA) walipokua wakifanya ukaguzi
kabla ya kuanza rasmi safari za kibiashara nchini.
Maafisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)wakilakiwa katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya ukaguzi kabla ya safari kwa ndege hizo kuanza.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ibrahim Mussa ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa
nchini(TANAPA) akizungumza na waandishi wa habari juu ya faida za utalii
zitakazotokana na kukua usafiri wa anga nchini.
Baadhi ya watumishi wa uwanja mdogo wa ndege wa Arusha wakifurahia ndege aina ya Bombadier baada ya kupata nafasi ya kuingia ndani ya ndege hiyo na kujionea mandhari yake.
Mkuu
wa kitengo cha usalama wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL) ,John Chaggu akijiandaa kuingia ndani ya
ndege kwa ajili ya kuendelea na ukaguzi katika viwanja vingine nchini ambavyo ndege hiyo itatoa huduma.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment