HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 24, 2016

Waandishi Mbeya wajadili mswada wa sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016

Wanahabari Mkoa wa Mbeya wakiwa katika Mkutano wa dharuara kwa ajili ya kujadili mswada wa sheria huduma za habari ya mwaka 2016 Mkutano huo ulifanyika jana katika Ofisi cha waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya aliye simama ni Mwandisghi kutoka Gazeti la Jambo Leo Moses Ng'wat.


NA KENNETH NGELESI, MBEYA

WAANDISHI wa habari Mkoa wa  Mbeya,wamewataka Wagunge wa Bunge la Jumuhuri ya Muungano wa Tanzania kuangalia upya  mswada wa  sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 kwa madai kuwa umelenga kuwakandamiza waandishi wa habari katika nyanja ya elimu ya shahada ya  juu.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya (MBPC)  Modestus Mkulu,katika Mkutano wa dharula wa waandishi wa habari ulifanyika katika Ofisi za chama hicho jiji hapa kwa ajili wa  kupitia  mapendekezo ya Mswada huo.

Akizungumza na waandishi walishiriki wa Mkuatano huo Nkulu alisema kuwa kuna vipengere  vingi vilivyopitishwa  vimelenga  kuwabana wanahabari katika suala zima la elimu  na kwamba  serikali ione namna ya kuwawezesha wanahabari kujiendeleza kielimu  ili kukidhi vigezo.

Katika hatua nyingine alishauri Serikali kupitia nakala za vyeti vya elimu kwa wabunge,watumishi  wa kada zingine na siyo kubana taaluma ya habari pekee kwani kuna baadhi ya wajiiriwa  wameishia elimu ya darasa la saba.

“Tuna watumishi wengi hawana elimu lakini wanatoa huduma vizuri na hata katika bunge wapo waliohitimu darasa la  saba sasa,wengine nagzia ya Cheti na Diploma  iweje mswada huu ubane  tasnia  ya habari pekee”alisema Nkulu
.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa (MBPC) Hosea cheyo ,alisema kuwa ipo haja kwa waziri mwenye  dhamana kuona njia mbadala ya kupunguza makali ya vifungu vya sheria kwa kutoangalia elimu ya ngazi ya shahada ya juu bali kwa utendaji wa kazi.

“Sio kwamba wanahabari hawataki kujiendeleza hoja hapo kama wote watakuwa na ngazi ya elimu ya shahada ya juu nani atamwongoiza mwenzake katika utendaji wa kazi “aliongeza Nkulu.
Naye  Moses Ng’wat mwandishi wa gazeti la Jambo Leo alisema kuwa vifungu vya sheria katika mswada huo  havijasimama kwa ajili ya kumtete mwandishi wa habari bali ni  kukandamizi  balia umelenga kuikandamiza tasnia ya habari hivyo ni vema waandishi wa habari na wadau wengine wa habari wakaujadili kwa kina mswada huo.

No comments:

Post a Comment

Pages