HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 28, 2016

WATATU NJE MBEYA CITY VS MAJIMAJI KESHO – Mbeya City Council FC

WAKATI kikosi cha mbeya City fc kikitarajiwa kushuka ndimbani  hapo kesho kucheza mchezo namba 98 wa ligi  kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya  Majimaji fc  ya Songea kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa,taarifa  imetolewa  kuwa nyota watatu wa kikosi hicho wataukosa mchezo huo  kutokana na kuuguza majeraha  waliyoyapata kwenye michezo  iliyopita.
Muda  mfupi uliopita Ofisa habari wa City, Dismas Ten,ameidokeza  mbeyacityfc.com  kuwa nyota watatu Ayoub Semtawa,John Kabanda na Omary Ramadhani hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho hii ni kwa sababu ya kupisha majeraha  waliyopata kwenye michezo mitatu ambayo City imecheza ikiwa nje ya uwanja wa nyumbani(Sokoine).
“Nimezungumza na dakatari wetu leo asubuhi, amenifahamisha kuwa hakuna uwezekano wa kuwatumia wachezaji Ayoub Semtawa, Omary Ramadhani na John kabanda kwa sababu bado hawajapona majeraha yao waliyoyapata kwenye michezo yetu iliyopita,kulikuwa na dalili na kupona kwa Omary lakini taarifa ya dakatari ndiyo hiyo hakuna uwezekano huo kwa sasa,” alisema.
Akiendelea zaidi, Ten alisema kuwa, Ayoub semtawa aliyeumia kwenye mchezo dhidi ya African Lyon atalazimika kukaa nje kwa wiki tatu zaidi kabla ya kurejea  uwanjani huku Kabanda na Omary wanaweza kuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa tarahe mbili dhidi ya Young Africans.
“Tunaweza kuwatumia Omary na Kabanda kwenye mchezo ujao lakini hakuna uwezekano wa Semtawa kurejea  uwanjani kwa sasa, daktari amesema atalazimika kukaa nje kwa majuma matatu zaidi hii ni kwa sababu alichanika nyama za paja ambazo zinahitaji muda kidogo wa mapumziko kabla ya kurejea”.
Katika hatua nyingine Ten aliweka wazi kuwa walinzi, Hassan Mwasapile na Haruna Shamte waliokuwa nje kwa majeraha tayari wamerejea kikosini na wamekuwa sehemu ya kikosi kwenye mazoezi ya siku tano yaliyofanika kwenye uwanja wa Sokoine kujiandaa na mchezo wa kesho hivyo hakuna shaka yoyote kuwa wanakuja kuimarisha safu ya ulinzi ya City.
“Taarifa nzuri kikosini ni kuwa Hassani Mwasapile na Haruna Shamte wanarejea kikosini, hili ni jambo jema kwa saababu wanakuja kuimarisha safu yetu ya ulinzi katika kuhakikisha tunaibuka na ushindi, uwepo wao utampa nafasi nzuri kocha wetu Kinnah Phiri kupanga kikosi ambacho  kitampa matokeo”, alimaliza.

No comments:

Post a Comment

Pages