HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 13, 2016

WAZIRI WA SHERIA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA TUME YA KUDUMU YA UCHUNGUZI

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI  wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi  (TKU) itakayofanyika Oktoba 21 mwaka huu katika Ukumbi wa Karimjee.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Makamu  Mwenyekiti wa Tume wa Haki za Binadamu na Tawala Bora,Idd Mapuri alisema  maadhimisho hayo yatakayayo washirikisha viongozi ,wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Alisema kongamano hilo  litakalojadili mada mbalimbali kuhusu utawala bora na utawala wa sheria nchini.

“Miongoni mwa mada zitakazowasilishwa ni pamoja na chimbuko,changamoto na mafanikio  ya TKU iatakayotolewa na Jaji Mstaafu wa Mahaka Kuu Gad Mjemmas , mada nyingine  ni uzoefu wa Afrik wa Taasisi za ‘Ombudsman’ itakayotolewa na muwakilishi kutoka Jumuiya ya Taasisi za Uchunguzi na Profesa Paramagamba Kabudi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)  atawasilisha  mada ya kutoka kwaTKU changamoto zilizopo na matarajio,”alisema Mapuri.
Aidha alisema Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damianu Lubuva atatoa hotuba itakayoeleza uzoefu wake TKU.

Alisema kauli mbiu ni “Utawala wa Sheria ndiyo msingi Mkuu wa utawala bora”.


No comments:

Post a Comment

Pages