Hatimaye wakazi wa mbagala
wanaofanya Biashara ndogo ndogo wakiwemo wajasiriamali wamepata neema kubwa
baada ya Bank ya AMANA kuzinduaa huduma yake mpya ya kutoa mikopo midogo midogo
kwa wafanya biashara, huduma ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es salaam ikiwa
ni miaka mitano Tangu kuanzishwa kwa Bank Hiyo.
Akizungumza na
wanahabari na wananchi wa mbagala ambapo ndio uzinduzi huo umefanyika
Mkurugenzi wa Bank Hiyo Dr Mosen Masoud amesema kuwa huduma hiyo imeanzishwa
mahususi kwa kutambua hitajio kubwa katika jamii la wafanya biashara wadogo
wadogo katika kupata mtaji ya kukuza biashara zao hivyo Bank ya Amana imeamua
kuwainua wafanya biashara hao wadogo ili kuinuka kipato chao na kufikia kipato
cha kati na hata kipato cha juu.
Amesema kuwa kupitia
huduma hiyo Amana Bank inawawezesha wafanya biashara kwa kununua bidhaa
wanazohitaji katika biashara zao na kuwauzia kwa bei nafuu kwa mkopo ambapo
watarejesha kidogo kidogo katika muda ambao umewekwa katika utaratibu.
Mkurugenzi wa Benki hiyo Dk. Mosen Masoud akizungumza na wanahabari na wananchi waliofika katika uzinduzi huo. |
Ameongeza kuwa wafanyabiashara
sasa wana nafasi ya kukodishwa vifaa mbalimbali wanavyohitaji katika kuendesha
biashara zao kwa kodi nafuu na mwishowe wanaweza wakanunua vifaa hivyo kwa Bei
nafuu
Mkurugenzi huyo
ameendelea kueleza kuwa kwa sasa Huduma hiyo ya mkopo imeanza kutolewa kwa
wateja wake wanaotumia Tawi lao la Mbagala tu lakini kusudi lao ni kuhakikisha
kuwa wanaendesha zoezi hiyo latika matawi yao yote nchini ambayo kwa sasa yapo
matawi saba.
Diwani wa Kata ya kibonde Maji mbagala Jijini Dar es salaam Mh Abdala Mtimika Akizungumza |
Akizunguza wakati wa
uzinduzi huo Mgeni Rasmi ambaye ni Diwani wa kata ya Kibondemaji Abdala Mtimika
ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Temeke amesema kuwa Uzinduzi wa Huduma
hiyo ya kutoa mikopo midogo modogo sasa imekuja wakati muafaka kipindi ambacho
watanzania wengi wamekuwa wakilalamika kudorora kwa uchumi na pesa kupotea hivyo
ni jukumu la wafanya biashara wa mbagala kutumia nafasi hiyo adhimi kuhakikisha
kuwa wanapata mikopo hiyo na kuwekeza katika Biashara zao.
Wiki ya Huduma kwa wateja ikiendelea wateja mbalimbali wakipata Huduma katika Tawi la Benk hiyo Mbagala leo. |
No comments:
Post a Comment