HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 30, 2016

MEYA WA JIJI LA ARUSHA AZINDUA KAMPUNI YA MASOKO YA KISMATY ADVERT MEDIA

Mkurugenzi wa Kismaty Advert Media Company Ltd, Bi. Mary Emmanuel Mollel akizungumza Machache katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 , 2016.
Mkurugenzi wa Kismarty Advert Media Company Ltd Mary Emmanuel ,akisalimiana na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.
Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.

Meya wa Jiji la Arusha amesema kuwa ni vyema kusapoti na kuyapa kipaumbele mambo mazuri yanayofanyawa na wazawa haswa kwa uthubutu wao wa kufanya mambo ya maendeleo 
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampuni ya matangazo inayojulikana kama Kismaty Advert Media company ltd , iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Asili Resort uliopo Jijini Arusha na kuhudhuriwa na wamiliki wa makampuni mbalimbali hapa nchini.



Meya huyo amewataka wananchi kuwa na tabia ya kutangaza biashara zao kwani bila kufanya hivyo hata kama bidhaa itakuwa na uzuri kiasi gani hakuna atakayefahamu thamani yake bila kuitangaza ndipo ifahamaike.



"Jengeni tabia ya kutangaza biashara zenu na bidhaa mnazokuwa nazo ndugu zangu biashara ni matangazo msikae kimya,ukizingatia hii ni kampuni ya kitanzania,tuache kukuza vya watu tutukuze vya kwetu ndugu zangu "alisema meya.



"Mnapoona kampuni kama hii ya matangazo ndiyo fursa yenyewe hii ya kuitumia kuzitangaza biashara zenu,ukikaa kimya hakuna mtu anayeweza kuifahamu bidhaa yako au biashara yako hata kama unauza vitu vizuri kiasi gani" alisema Meya.



Kwa pande wake mkurugenzi wa Kismaty Advert Media Company ltd ,Bi. Mary Mollel amesema kuwa kampuni hiyo inapokea matangazo ya aina mbalimbali na Kuyasimamia kwa ukaribu na kwa bei ambayo mteja atakayoimudu .



Hivyo amewataka wafanyabiashara biashara mbalimbali kutokuwa waoga kutangaza biashara zao kwani ndiyo njia pekee itakayowasaidia biashara zao kufahamika zaidi na kupata wateja zaidi.



"Msiwe waoga kuthubutu kutangaza biashara zenu hapa tunasaidiana wewe unaleta tangazo nakutangazia kwa bei nzuri na wakati huohuo unapata wateja kwa upande wako ,kwa maana nyingine tunawezeshana karibuni sana. " alisisitiza Bi Mary.

No comments:

Post a Comment

Pages