Vyombo vya baadhi ya wakazi wa nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam vikitolewa nje baada ya wamiliki wa nyumba kushindwa kulipia nyumba hizo kwa mujibu mikataba waliyokubaliana na Shirika hilo. (Picha na Francis Dande).
NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendelea na kazi
ya kuwaondoa wadaiwa sugu.
Wadaiwa hao ni wale walionunua nyumba na kushindwa kulipa deni
lililobaki kwa muda uliopangwa.
Akizungumza jjijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mipango
na Uwekezaji wa NSSF, Radhia Tambwe, alisema kwamba nyumba hizo ni za Mtoni
Kijichi.
Radhia alisema kwamba kazi hiyo itafanyika kwa wadaiwa saba.
“Wakazi wa nyumba zote hizo walitolewa na kampuni ya udalali
ya Majembe Action Mart kwa kushirikiana na NSSF,”alisema.
Aidha alisema kwamba wadaiwa hao waliondolewa katika nyumba
hizo baada ya taratibu za kisheria kufuatwa hivyo nyumba hizo zitauzwa kwa watu
wengine.
Aidha alisema kwamba kazi hiyo ni endelevu kwa wale
watakaoshindwa kulipa madeni yao kama mikataba inavyosema.
Shirika la NSSF limewataka walionunua ama kupanga nyumba
kulipa kwa mujibu wa mikataba yao ili kuepuka adha ya kutolewa vyombo vyao nje
na kupata hasara.
No comments:
Post a Comment