Rais wa Zanzibar Dk Shein akisaini sheria ya Mafuta na Gesi zanzibar.
Na Talib Ussi, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhammed Shein amesaini Mswada wa sheria ya mafuta na Gesi na kudai hajavunja katiba ya muungano na kueleza kuwa kunawanasheria wameona kavunja wachukue hatua wanazozijua dhidi yake.
Alieleza kuwa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anaiheshimu na kudai alichokifanya amekifanya kwa mujibu wa sheria ilitungwa na kupitishwa na Bunge ambayo ni sheria namba 21 ya mwaka 2015.
Dk. Shein aliyaeleza hayo Visiwani hapa Ikulu wakati aliposaini mswada wa sheria ya mafuta na kuifanya kuwasheria kamili ambayo itatoa fursa ya kuendeleza Nishati ya Mafuta na Gesi.
“Kama wao ni mabingwa wa katiba na wameona nimevunja katiba ya Muungano basi wachukue hatua wanazozijua” alieleza Dk. Shein.
Alieleza kuwa hakuna katiba aliyovunja na alichokifanya ni halali kwa mujibu wa Sheria ya Jamuhuri ya Mungano ya Mafuta na Gesi ya 2015 ambayo alidai inaipa mamlaka Zanzibar kuazisha sheria yao.
“Nimesaini sheria hii baada ya mashauriano makubwa kati ya Wanasheria wakuu wa serikali mbili ya Mungano na SMZ kwa muda mwingi” alifahamisha Dk. Shein.
Alieleza kuwa katiba ilipitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano na Sheria hio imetungwa na bunge hilo kwa hio haoni kuwa yeye kafanya makosa.
Kwa mujibu wa wanasheria sheria hio italeta utata mkubwa ambao utapelekea kampuni zilizo makini kusitisha azima ya kuwekeza katika Nishati hio.
Akizungumza na Tanzania daima Mwanasheria wa Kujitegemea Omar Said Shabaan alieelza kuwa mgogoro wa kwanza nni kuwa bado suala la mafuta na gesi ni mambo ya Muungano, ambapo alikielezea kifungu cha 64 (30).
Alieleza kuwa Katika Ibara hiyo imetoa katazo kwa baraza la wawakilishi kutunga sheria yoyote inayohusu jambo loloote ambalo chini ya mamlaka ya Bunge na kuendela kuwa katika iliweka wazi kuwa ikiwa jambo hilo litafanyika basi sheria hiyo itakuwa batili.
“Wanafanya sheria hicho kwa madaie eti kufungu cha 2 cha sheria mafuta na gesi ya jamuhuri ya Muungano ndio kinachowapa malaka hio hapana, kwa mujibu wa kifungu hichi Zanzibar inatakiwa kuazisha taasisi ambayo itakuwa chini ya sheria na kanuni zinazotokana sheria ile sio kuazisha zao” alieeza Shaabani.
Alieeleza kuwa wanapewa mamlaka ya kuazisha taasisi ambayo itasimamia (ZPDC) hizo sheria na kanuni ambazo zinatakana sheria ya mafuta na gesi.
FUNGU MBARAKA.
Dk. Shein amevunja ukimya na kusema kuwa kisiwa cha Fungu mbaraka ni mali ya Zanzibar na kudai kuwa dunia yote ina elewa hivyo.
“Sisi tunaamini Kisiwa cha Fungu mbaraka ni cha kwetu na hakuna ambaye anaweza kudai kuwa ni cha kwao” alieelza Shein.
Alisema kama kuna mtu anadai ni cha kwake aiandikie rasmini SMZ na wao watamjibu wanaushahidi wa kila aina kuwa ni cha Zanzibar.
No comments:
Post a Comment