HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 15, 2016

TANESCO YAAHIDI UMEME WA UHAKIKA KATIKA TANZANIA YA VIWANDA

Ziara ya hivi karibuni ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, alipotembelea kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
KUONGEZEKA kwa shughuli za Kiuchumi pamoja na ongezeko la idadi ya Watu waliopatiwa Huduma ya umeme Nchini, kumefanya mahitaji ya umeme kuwa makubwa zaidi.

Mathalan takwimu zinaonesha, mahitaji ya juu ya umeme yameongezeka kutoka MW 988.27 Mwezi Desemba 2015 hadi kufikia MW 1,026.02 Mwezi Machi, 2016 sawa na ongezeko la asilimia 4.

Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la Umeme Nchini Tanzania (TANESCO), imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuboresha Miundombinu ya umeme kote Nchini ili Wananchi waweze kupata umeme ulio bora na wa uhakika zaidi na hivyo kuemdana na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imedhamiria kujenga uchumi wa Viwanda.

Miongoni mwa hatua ambazo TANESCO imekuwa ikichukua ni pamoja na kukarabati na kubadilisha Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji umeme kwenye maeneo kadhaa ya Nchi.

Hali ya upatikanaji umeme Nchini kwa sasa imeendelea kuimarika siku hadi siku ukiachilia mbali katika baadhi ya maeneo Nchini ambayo umeme hukosekana kwa sababu ya hitilafu za muda mfupi pamoja na matengenezo yanayoendelea hivi sasa kote nchini ya kukarabati na kubadilisha Miundombinu ya umeme.
Kwa sasa uwezo wa mitambo ya kufua umeme (installed capacity) Nchini ni MW 1,439.97 ambapo MW 1357.69 ni mitambo iliyounganishwa katika Gridi ya Taifa na kiasi cha MW 82.28 ni mitambo iliyo nje ya Gridi (Isolated stations).Uwezo wa mitambo ya kufua umeme katika Gridi ya Taifa kwa kutumia nguvu za maji (hydropower)  ni MW 566.79 sawa na asilimia 41.70 ya mitambo yote. Mitambo itumiayo Gesi Asilia ni MW 607.00 sawa na asilimia 44.7 wakati Mitambo ya kufua umeme kwa kutumia mafuta ina uwezo wa MW 173.40  sawa na asilimia 12.8, na umeme unaofuliwa kwa kutumia biomass ni MW 10.5 sawa na asilimia 0.8 ya mitambo yote.

No comments:

Post a Comment

Pages