HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 16, 2016

SSRA ILIPOSHIRIKI MAONESHO NA KONGAMANO LA HUDUMA ZA KIFEDHA KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE JIJINI DAR ES SALAAM

Mgeni rasmi katika maonesho ya huduma za kifedha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustine Kamuzora akipata maelezo kuhusu shughuli za Mamlaka kutoka kwa Afisa wa SSRA, Ally Masaninga, Maonesho yaliyoandaliwa na Kampuni ya Mikono Speakers katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha uhusiano na Uhamasishaji cha SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika akifafanua jambo alipokuwa akitoa mada ya Hifadhi ya Jamii katika kongamano la huduma za Fedha lililoandaliwa na Kampuni ya Mikono Speakers hivi karibuni.
Baadhi ya wadau walioshiriki wakisikiliza mada ya Hifadhi ya Jamii toka kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakitoa maelezo na huduma zinazofanywa na Mamlaka katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, sambamba na Kongamano lililokuwa likifanyika katika ukumbi wa huo, hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Pages