Na Talib Ussi, Zanzibar
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif sheriff Hamad amesema Demokrasia iliyofanywa marekani ni aibu kwa Nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania katika kuendesha chaguzi zao.
Maalim Seif ambaye alitembelea marekani wakati wa kampeni za uchaguzi huo ulifanyika wiki iliyopita alieleza kuwa hakuona vyombo vya vikiingilia shughuli za kampeni wale uchaguzi wenyewe tofauti ilivyo kwa nchi nyingi za Kiafrika.
Maalim aliyasema hayo katika mazungumzo maalum na vyombo vy habari huko Nyumbani kwake Mbweni visiwani hapa.
Alisema Nchi kama Marekani yenye wapiga kura zaidi ya 45 milioni ndani ya masaa 24 walipiga kura na kupata matokeo yake.
Alisema kwamba amekuwa akishangaa kwa nchi kama Zanzibar ambayo ina wapiga kura laki nne lakini huchukuwa siku tatu kutangaza matokeo.
“Marekani wiki iliyopita sote tulishuhudia kuwa watu zaidi ya milioni 40 walipiga kura na ndani ya masaa 24 wakaweza kutangaza matokeo kinyume na Zanzibar ambayo watu wake hawazidi laki tano lakini iankuwa muda mrefu kutangazwa matokeo yake”, alisema.
Hata hivyo alisema kwamba kitendo cha Marekani kinapaswa kutiliwa maanani na ni funzo kubwa kwa nchi zote za kiafrika hasa Tanzania na Zanzibar.
Kwa upande wa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC), amesema kuwa kuna mtu najigamba kwamba chombo hicho hakina uwezo wa kuingilia maamuzi mamlaka ya Zanzibar dhidi ya uchaguzi.
Alisema yeye na viongozi wenzake walipeleka shauri lao ICC la uvunjifu wa haki za binadamu uliofanywa na utawala wa mabavu Zanzibar na Tanzania kwa ujumla
“Kama anajidai yeye haogopi ICC basi asubiri sisi tumeshawakabidhi mawakili wetu na tayari wamefika katika hatua nzuri”, alisema Maalim Seif.
Hivi karibuni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa kisiwani Pemba alitamka kwamba chombo hicho cha ICC hakina uwezo wan kuingilia uchaguzi uliopita.
Maalim Seif alisema mtu huyo hajui lolote dhidi ya ICC na muda wake ukifika atakwenda kujibu mbele ya mahakama hiyo.
No comments:
Post a Comment