*TAWI JIPYA LA CHUO KIKUU CHA SAUTI ARUSHA LAZINDULIWA
* WASOMI 165 WAJIUNGA CCM KWA KUVUTIWA NA UTENDAJI WA JPM
* SHIRIKISHO BADO HALILIRISHWI NA KASI YA BODI YA MIKOPO
Na Mwandishi Maalum
VIONGOZI wa ngazi ya juu kutoka makao makuu ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Hamidu Mhina (M-NEC), katika Kanda ya Kaskazini, imemalizika kwa mafanikio makubwa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu Msaidizi wa CCM, ambaye ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho hilo la Vyuo vya Elimu ya Juu, Daniel Zenda amesema, miongoni mwa mafanikio yaliyojiri katika ziara hiyo ni kuingiza wanachama wapya 165 ambao ni wasomi kutoka Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT).
Zenda alisema, wasomi hao waliamua kujiunga CCM, kutokana na kuwa na imani na utendaji kazi wa Menyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli ambapo wameeleza kuwa na matumaini ya nchi kupiga hatua kubwa kimaendeleo chini ya Rais Magufuli. Alisema, mapokezi ya wanachama hao wapya yalienda sambamba na uzinduzi wa tawi jipya la CCM la SAUT.
Alisema, pia katika ziara hiyo, Shirikisho liliazimia kuzindua Maktaba Maalum ya Kidigitali " Online library" ambayo itakuwa huduma zake bure na itajumuisha vitabu vyote vikiwemo vya lugha ya Kiswahili. "Maktaba hii itaisaidia usomaji wa vitabu kupitia mtandao na itarahisisha upatikanaji wa vitabu na kuongeza maarifa zaidi kwa Wasomi na hata Wakufunzi/Walimu. Shirikisho itazindua library hiyo hivi karibuni". amesema Zenda.
"Kaika ziara hii tuli tulijadiliana na wananchama kuhusu hali ya kisiasa sambamba na hali ya utoaji mikopo kwa wanafunzi. Shirikisho limebaini bado changamoto kuhusu mikopo bado zipo zipo hasa mikoani, hivyo tumewaomba watumishi wa bodi ya Mikopo kuongeza kasi ya kushughulikia matatizo hayo na kwa upande mwingine wakuu wa Vyuo kuhimiza majina ya wanafunzi/Wanufaika wa mikopo kuwasilishwa haraka kwenye Bodi kama alivyosema Waziri, mwenye dhamana ya elimu Prof Joyce Ndalichako"Alisema.
Alisema, pia katika ziara hiyo, viongozi walikagua uhai wa Shirikisho matawini na mikoani na kuwataka kila mwanachama kutimiza wajibu wake kama ilivyoainishwa ndani ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha shirikisho linakuwa kimbilio la wanafunzi hasa katika Matawi katika kutatua changamoto zilizopo Mavyuoni.
Zenda alisema pia Shirikisho Taifa limewakumbusha Wanachama wake Wasomi kuendelea na kuongeza nguvu katika kukisemea Chama Chao cha CCM, pamoja na Kazi Kubwa anayoifanya Rais Dk. John Magufuli kutekeleza ahadi na ilani ya CCM ikiwemo Ongezeko mikopo ya Vyuo vikuu, Kubaini mikopo hewa, Elimu bora, Elimu bure, Kubaini Wanafunzi hewa hivyo kuokoa fedha nyingi.
" Katika ziara hii tulidhihirisha shukrani na pongezi za Shirikisho kwa Mwenyekiti wa CCM, Dk John Magufuli, kwa kukomesha matumizi yasiyo ya lazima, kusimamia vema kodi, Uwajibikaji, Maadili ya Utumishi wa Umma na ununuzi wa ndege mpya za kisasa.
Zenda alisema, pia katika ziara hiyo viongozi walitumia fursa hiyo kutangaza nafasi ya Mwenyekiti wa Shirikisho mkoa wa Kilimanjaro kuwa wazi na hivyo wanachama wa CCM wanaohitaji nafasi hiyo, kuwa tayari kugombo nafsi hiyo pindi uchaguzi utakapowadia.
Alisema, pia ziara hiyo ilijikita kuelekeza kufanyika kwa uhakiki wanachama waliopo na kupokea taarifa za kiutendaji pamoja changamoto zilizopo mikoani pamoja na Kutoa rai juu ya Wanachama Hewa na kuelekeza Uhakiki ufanyike kuanzia ngazi ya Matawi.
"Shirikisho Taifa limehamasisha na kuwataka Wanachama waliomaliza masomo kujiunga kwenye vikundi ili kushiriki katika Programu ya Uzalendo "UZALENDO NI VITENDO" ili kujitolea kufanya shughuli za kimaendeleo na kutoa mchango katika Taifa. Mfano Ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo ya shule pamoja na mabweni na nyumba za Walimu", Alisema Zenda.
Katibu Msaidizi wa CCM, ambaye ni Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Daniel Zenda akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, kuhusu ziara hiyo ya Kanda ya Kaskazini, Wengine Kushoto ni Katibu Uhamasishaji wa Shirikisho hilo Mganwa Nzota na Makamu Mwenyekiti w Shirikisho hilo (M-NEC CCM), Hamid Mhina.
No comments:
Post a Comment