Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko
wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida aliyeshikilia Tuzo katika picha ya pamoja na
watumishi wa Mfuko mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya ushindi wa kwanza ya Ufungaji
bora wa mahesabu ya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2014/15. Hafla ya kukabishi tuzo
hizo zilifanyika tarehe 03/12/2016 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko
wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida akipokea Tuzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu
Bw. Eliud Sanga wa ufungaji bora wa
mahesabu kwa mwaka 2015 kutoka kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
Bw. Shogolo Msangi. LAPF iliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko
Bw. John Kida akiwa ameshikilia Tuzo, pamoja nae ni timu ya Kurugenzi ya Fedha ambayo kwa
kiasi kikubwa ndiyo ilifanikisha ushindi huo wa ufungaji bora wa mahesabu kwa
mwaka wa fedha 2014/15 LAPF imekuwa mshindi wa kwanza mara sita kati ya mara nane tangu kuanzishwa kwa
Tuzo hizo zilizoasisiwa na NBAA mwaka 2008.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko
wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida akipongezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA
Pro. Isaya Jairo kwa ushindi wa kwanza wa ufungaji bora wa mahesabu ya Mfuko
kwa mwaka wa fedha 2014/15. Tuzo hizo zilitolewa tarehe 03 Disemba, 2016.
No comments:
Post a Comment