HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 26, 2016

WAZIRI WA HABARI AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA MPOKI BUKUKU

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa Kampuni ya The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku nyumbani kwake Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam leo. Bukuku anatarajiwa kuzikwa Desemba 27 katika makaburi ya familia yaliyopo nje kidogo ya mji wa Dodoma eneo la Msalato. Marehemu Bukuku alifariki Desemba 23 baada ya kugongwa na gari katika eneo la Mwenge wakati akitoka kazini. (Picha na Francis Dande)
Waziri Nape (katikati), akiwa na Wakili Nyaronyo Kicheere (kushoto), na Mpiga Picha wa Magazeti ya MCL, Edwin Mjwahuzi nyumbani Tabata Kimanga.
Wanafamilia.
Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akimpa pole mke wa marehemu, Lilian Mpoki alipoenda kuifariji familia hiyo nyumbani Tabata.
Waombolezaji.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa Kampuni ya The Guardian Ltd, Marehemu Mpoki Bukuku katika uwanja wa Shule ya Msingi Wazazi Tabaga Kimanga Dar es Salaam. 
Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Mpiga Picha Mwandamizi wa Kampuni ya The Guardian Ltd, Marehemu Mpoki Bukuku.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho katika ibada ya kuaga mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.
Mwandishi wa Habari Freddy Maro akitoa heshima za mwisho.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akitoa salamu za rambirambi kwa wakati wa kuaga mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.

 Mwenyekiti wa Chadema akitoa salamu za rambirambi katika msiba huo.
 Familia ya Mpoki Bukuku ikiwa mbele ya jeneza lake.
 Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho.
 Mfanyakazi wa Kampuni ya The Guardian, Halima Kambi akitoa heshima za mwisho.
 Wanahabari wakipita na kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la marehemu Mpoki Bukuku.
 Mbunge wa Ubungo, Sayed kubenea akitoa heshima za mwisho.
Wengi walishindwa wa kujizuia na kuangua vilio wakati wa kuaga mwili  Mpoki Bukuku.
 Wanahabari wakitoa heshima za mwisho.
Waandishi wa habari wakitoa heshima za mwisho.

 Mke wa marehemu Lilian akitoa heshima za mwisho kwa mume wake marehemu Mpoki Bukuku.

No comments:

Post a Comment

Pages