MAMLAKA ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) yatwaa ushindi wa NBAA katika
utunzaji bora wa mahesabu kwa mwaka 2014/15. SSRA imekuwa mshindi wa pili kati
ya Mamlaka za Udhibiti zinazotumia viwango vya Kimataifa vya mahesabu ya
Taasisi za Umma (IPSAS).
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bibi. Irene
Isaka akipokea Tuzo ya NBAA ya utunzaji bora wa mahesabu ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Mwenyekiti
wa Bodi ya SSRA Bw. Juma A Muhimbi aliyeshikilia Tuzo ya NBAA baada ya SSRA
kuibuka mshindi katika utunzaji bora wa mahesabu wengine pichani ni watumishi
wa Mamlaka.
Bw.
Juma Muhimbi, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi
ya Jamii akimpongeza Bibi. Irene Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA.
Bi.
Latifa Mazengo, akiwa ameshikilia Tuzo hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bibi Irene
Isaka akiwa pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo.
No comments:
Post a Comment