Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Moses Nnauye, (wapili kushoto), akipokea fomu ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bw. Adam Mayingu, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Bolggers Tanzania, (TBN), uliomalizika jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa TBN, Bw. Joachim Mushi.
Waziri Nape, akipokea kadi yake ya kujiunga na Mfuko huo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
NA K-VIS MEDIA/KHALFAN
SAID
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Moses
Nnauye, amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF na kuusifu kwa huduma zake za
haraka.
Waziri Nape, amejiunga muda mfupi baada ya kufunga Mkutano Mkuu
wa Mwaka wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), kwenye jingo la kitega uchumi
la Jubilee Towers linalomilikiwa na Mfuko huo jana.
Aidha washiriki wa mkutano huo nao pia walijiunga na Mfuko huo
kupitia uchangiaji wa Hiari yaani PSS.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi yake ya uanachama
iliyotengenezwa chini ya dakika 15, Waziri Nape alisema, “Aise, kitambulisho change
tayari, hongereni sana kwa huduma za haraka, mimi sikujua kama mnafanya kazi
kwa kasi yanamna hii,” alisema Mh. Nape wakati akikabidhiwa kadi hiyo na Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi ofisini kwake.
Tangu kujaza fomu, kupiga picha na kukabidhiwa kitambulisho
hicho, Waziri alitumia kiasi cha dakika 25 tu, ikiwa ni muda mfupi baada ya
kufunga mkutano huo.
Nao wanachama wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), waliokuwa
wakishiriki mkutano huo, wamejiungana PSPF, baada ya kupatiwa maelezo ya kina
kuhusu umuhimu wa kujiunga na Mfuko, kutkana na manufaa mengi ukiachilia mbali
kujiwekea akiba.
“Ukiwa Mwanachama wa Mfuko, moja ya faida kubwa ni kujipatia
bima ya Afya, itakayokusaidia wewe na familia yako, nikiwa na maana ya mke/mume
na watoto,” alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdyul Njaidi katika
mada yake aliyoitoa kwa washiriki kuhusu kazi za Mfuko huo.
Waziri Nape, akijaza fomu hiyo, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu na kulia ni Bw. Njaidi.
Bw. Njaidi akitoa mada kuhusu kazi za Mfuko huo kwa washiriki wa mkutano wa TBN.
Bw. Njaidi akitoa mada kuhusu kazi za Mfuko huo kwa washiriki wa mkutano wa TBN
Washiriki wa Mkutano wa TBN, wakijaza fomu, huku Bw. Njaidi akitoa maelezo zaidi kwa baadhi yao
Bw. Mayingu akimkabidhi zawadi Waziri Nape
Waziri Nape, baadhi ya wafadhili wa mkutano kutoka PSPF, na NMB, wakiwa aktika picha ya pamoja na baadhiya washiriki wa mkutano huo wa TBN
Mmiliki wa Blogu ya Libeneke la Kaskazini kutoka Arusha Bi. Woinde Shizzah akijaza fomu za kujiunga na PSPF
Baadhi ya washiriki wakijaza fomu za kujiunga na PSPF.
Waziri Nape akimkabidhi Bw. Seria Tumainieli kadiya kujiungana PSPF
Waziri akimkabidhi Bi. Veronika kadi ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Waziri akimkabidhi Bw. Gadiola Emmanuel kadi ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
No comments:
Post a Comment