HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 07, 2016

Trump akataa ndege mpya za Air Force One

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amesema anataka kufuta ombi la ununuzi wa ndege mpya za Air Force One ambazo hutumiwa na marais wa Marekani.
Wiki sita kabla yake kuingia madarakani, aliandika kwenye Twitter: "Boeing wanaunda ndege mpya aina ya 747 Air Force One za kutumiwa na marais siku zijazo, lakini gharama yake imezidi, zaidi ya $4 bilioni. Futa oda hiyo!"
Serikali ya Marekani iliingia kwenye mkataba na kampuni ya Boeing wa kuundwa kwa ndege mbili au zaidi za kuwabeba marais.
Ndege hizo zilitarajiwa kukamilika na kuanza kutumiwa mwaka 2024.
Hisa za kampuni hiyo ya ndege ya Boeing zilishuka kwa zaidi ya 1% baada ya ujumbe huo wa Trump kwenye Twitter, ingawa zilijikwamua baadaye alasiri.
Bw Trump hatarajiwi kutumia ndege hizo mpya, iwapo hatashinda uchaguzi wa muhula wa pili mwaka 2020. 
CHANZO BBC. 

No comments:

Post a Comment

Pages