Ametoa
agizo hilo leo (Jumanne, Desemba 6, 2016) alipotembelea Ofisi za makao makuu ya
NCAA, zilizoko wilayani Ngorongoro mkoa Arusha wakati akizungumza na
watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa
ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani hapa.
"Nina
taarifa zenu kuwa mlimuhamisha kwa siri faru John kreta na
kumpeleka V I P Grumet Serengeti Disemba 17, 2015 na mliahidiwa
kupewa sh. milioni 200 ambapo mkapewa sh. milioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa sh. milioni 100
nyingine baadaye,".
“Naomba
niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua
zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe ziletwe
ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu wahusika wote
watachukuliwa hatua kali za kisheria,”.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu apega marufuku tabia ya baadhi ya watumishi wa
mamlaka hiyo ambao wanawakabidhi watoto kupeleka ng’ombe wao ndani ya kreta. “
Watumishi wa Ngorongoro ndiyo wanaopeleka ng’ombe ndani ya kreta na si wenyeji.
Sasa marufuku na tutakayemkuta hatutakuwa na msamaha naye,”.
Amewataka
watumishi hao kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wanafanyakazi kwa kufuata
misingi ya kiutumishi na kuacha tabia za kuendekeza rushwa na wizi.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa NCAA, Sezzary Simfukwe
kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili na tayari anahojiwa
na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
"Haiwezekani
mtumishi awe anachunguzwa na TAKUKURU halafu aendelee kuwa ofisini
si atavuruga uchunguzi. Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi
utakapokamilika na aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini,” alisema.
Pia
Waziri Mkuu alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa NCAA, Fred Manongi kueleza zilipo sh.
bilioni moja zilizotolewa na Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete kwa
ajili ya kujengea ranchi ya wafugaji wa tarafa ya Ngorongoro.
Akijibu
swali hilo Manongi alisema wakati Rais Kikwete anatoa fedha hizo alikuwa bado
hajateuliwa kushika washifa huo, ambapo Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi huyo kufanya
uchunguzi juu ya fedha hizo na kasha kumpelekea tarifa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, DESEMBA 6,
2016.
No comments:
Post a Comment