MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa
Mbaruku (pichani )amewataka madereva wa pikipiki maarufu kama
bodaboda jijini
Tanga kuacha kuendesha mwendokasi kwani maisha ya watu yanapotea
kwa sababu yao.
Sambamba na hilo amewataka kuondokana
na tabia ya kupakia abiria zaidi ya mmoja wanapokuwa barabarani maarufu kama
mshikaki kwani jambo hilo ni hatari kwa mustakabali wa maisha yao wanapokuwa
njiani.
Mbunge huyo alitoa wito huo
wakati akizungumza na madereva wa pikipiki Kata ya Kirare Jijini Tanga ikiwa ni
muendelezo wa ziara yake ya kuwatembelea wananchi na kuangalia changamoto
zinazowakabilia kasha kuona namna ya kuzipatia
ufumbuzi.
Aliwataka pia kutii sheria za usalama
kwa kuvaa kofia ngumu na kuacha kuwa na mbwembwe wanapokuwa barabarani jambo
ambalo linaweza kusababisha ajali zinazoweza kugharimu maisha ya
watu.
“Lakini pia madereva wa bodaboda
hakisheni mnakuwa nadhifu kwa wateja wenu pendeni kazi ikiwemo kuacha kuvaa
malapa badala yake wavae viatu vya ngazi “Alisema mbunge
huyo.
Hatua ya mbunge hiyo inatokana na
kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya waendesha bodaboda hao kuwa wamekuwa
wakikamatwa na askari wa usalama barabarani wanapokuwa kwenye shughuli zao
jambo ambalo linasababisha kushindwa kufikia malengo
yao.
Bakari Juma ambaye ni mwendesha
bodaboda eneo hilo alisema kuwa wamekuwa wakikumbana na wakati mgumu katika
kufanya shughuli hizo kutokana na kukamatwa mara kwa mara na kutakiwa kutoa
faini.
Naye Zuberi Omari alimuomba mbunge
huyo kuangalia namna ya kuwasaidia waendesha bodaboda hao ili waweze kujikwamua
kiuchumi kwa kuanzisha chama cha kukopa na kuweka akiba (Saccos) yao
ambayo inaweza
kuwa mkombozi.
Alisema hivi sasa baadhi ya watu
mbalimbali wamekuwa wakianzishya vikundi mbalimbali vikiwemo vya kukopa na
kuweka fedha hivyo nasi tungeweza kupata fursa hiyo ingeweza kutusaidia
kukabiliana na ugumu wa maisha.
Akizungumzia suala hilo, Mbunge Mussa
alisema lazima wahakikisha wanaheshimu sheria za usalama barabara kwa kuacha
kuendesha mwendokasi ikiwemo kuwa na leseni za kufanya shughuli hizo ili kuweza
kuzifanya kwa usalama zaidi bila kuwepo kwa
usumbufu.
Mussa aliwataka pia kuacha kutumia
mtindi wa kupakia abiria zaidi ya uwezo wanaakiwa kuwapakia wanaopokuwa kwenye
shughuli hizo maarufa kama mshikaki kwani madhara yake ni makubwa sana kwa
usalama wao na abiria hao kwani wanaweza kukumbana na ajali ikiwemo kugharimu
maisha yao.
“Leo hii ukiangalia wapo watu ambao
wanaendesha vyombo vya moto kama vile bodaboda hawavai elementi lakini
wanapakia abiria mishikaki sasa hawa wanakuwa na hatari kubwa kwa usalama
barabarani hivyo niwatake muache suala hilo
“Alisema.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment