Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakam Kuu Tanzania Jaji Ferdinandi Wambali (kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Na Benjamin
Sawe, Maelezo
Rais
John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho
ya siku ya Sheria nchini zitakazofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika viwanja
vya Mahakama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma
amesema mahakama itawaelimisha wananchi jitihada mbalimbali ilizochukua zenye
lengo la kuboresha huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano inaoutekeleza
katika kutoa haki kwa wakati na kuwezesha ukuaji wa uchumi.
Amesema
kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, mahakama itafanya matembezi maalum
yatakayoongozwa na Rais Mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi na yataanzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
na kuishia katika viwanja vya Mnazi mmoja
Katika
matembezi hayo Mhe. Rais Mstaafu Mwinyi atazindua rasmi maadhimisho ya wiki ya
elimu ya sheria ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuelekea maadhimisho ya kilele
cha siku ya sheria nchini.
Aidha
ametoa rai kwa wananchi kutembelea sehemu zote zilizoandaliwa kwa ajili ya
utoaji elimu ya sheria nchini kwa ajili ya kujifunza na kupata huduma
mbalimbali za Kisheria
Alizitaja
huduma hizo ni pamoja na taratibu za ufunguaji mashauri katika ngazi mbalimbali
za mahakama, taratibu za kesi za mirathi, taratibu za kesi za dhamana, taratibu
za rufaa, ndoa na talaka, taratibu za kupokea na kushughulikia malalamiko na
Msaada wa Kisheria
Maadhimisho
ya Siku ya Sheria nchini hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa pili na
mwaka huu yamebeba ujumbe wa Umuhimu wa Utoaji Haki kwa Wakati Kuwezesha Ukuaji
wa Uchumi.
No comments:
Post a Comment