Mchezaji wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Vicky Elias (wa kwanza kushoto), akipiga mpira wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya maadhimisho ya miaka 10 ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Salim Mwanyenza na Hawa Wanyenche. (Picha na Lutei Selemani Semunyu).
IDADI ya Wanawake wanaojiandaa na mashindano ya miaka 10 ya klabu ya golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imeongezeka na kuongeza joto la maadhimisho ya klabu hiyo yanayotarajiwa kufanyika mwezi Februari Jijini Dar es salaam.
Mmoja wa wachezaji hao ni aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Wanawake Hawa Wanyenche ambaye kwa muda mrefu hakuwa akionekana viwanjani kucheza lakini sasa ameibukia katika klabu ya Lugalo.
Akizungumza wakati wa mazoezi yake katika klabu ya lugalo Hawa alisema anaona kiwango chake kinaanza kurejea kutokana na kutokuwa uwanjani muda mrefu na anaamini kuibuka na ushindi katika mashindano hayo na yeyote yajayo ili kurejesha heshima yake.
“ Unajua ni muda mrefu sijaingia uwanjani na falsafa yangu ni kuishinda sio kushindwa na siri ya kushinda ni mazoezi ndio maana nimeanza mapema hivyo wanawake wengine wanajua wako vizuri katika golf waje tupambane”. Alisema Hawa.
Aliongeza kuwa ni wakati muafaka kwa Wachezaji wengine wa Vilabu vingine nao kujipanga na kuhakikisha wanashiriki ili kufanikisha mashindano lakini pia kuzihirisha uwezo wao.
Naye Mchezaji Vicky Elias alisema muda umekwisha na ukizingatia kuna uwezekano wa wachezaji kutoka katika nchi mbalimbali kuja kushiriki michuano hiyo hivyo mazoezi pekee ndio yatakayowafanya kuibuka na Ushindi.
“ Wachezaji wengi wamekamia mashindano haya lakin I nitashinda ingawa nikishindwa nitakubaliana kwa kuwa ni moja ya matokeo katika Golf kwani mchezo huo hautabiriki” Alisema Vicky.
Kwa Upande wake mchezaji Chipukizi Habiba Likuli alisema kikubwa ni kukabiliana na ushindani na kuibuka na ushindi na kulibakiza kombe la historia kwa klabu.
“ Mashindano yaliyopita nilicheza katika kundi la Watoto Junior lakini kutokana naKiwango changu ninaimani nitakuwa na uwezo wa kuchezea kundi la Wanawake Ladies katika mashindano hayo kama kanuni zitaruhusu” Alisema Habiba.
Kwa upande wake Kapteni wa Klabu ya golf ya Lugalo Kapteni Japhet Masai alisema katika kuyapa uzito mashindano hayo wamepeleka mialiko katika nchi za Zambia,Kenya,Malawi, Zimbambwe, Rwanda na Uganda.
Aliongeza kuwa tarehe na mgeni Rasmi katika Mashindano hayo anatarajiwa kutangazwa na mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Jumanne saa nne katika Klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment