NA MWANDISHI WETU
BENKI M
Tanzania, imefunga mwaka wa fedha wa 2016 kwa kasi ya aina yake kwa kupata
ongezeko kubwa la rasilimali zake kufikia
kiasi cha trilioni 1 mwishoni mwa
mwaka 2016.
Kwa mujibu
wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Bi. Jacqueline Woiso, ni moja ya mafanikio makubwa kwa benki hiyo.
“Mafanikio
ya Benki kwa mwaka 2016, yamekuwa mazuri sana. Kwa ujumla, yanatupa matumaini makubwa na tunavyouanza mwaka huu mpya, tukiamini utakuwa wa mafanikio
makubwa,” alisema.
Kuhusu
rasimali za Benki, Bi. Woiso alisema
zimeongezeka kutoka bilioni 977.66 kwa mwaka 2015 hadi 1,051.89 bil mwishoni
mwa mwaka 2016.
Alisema
mapato ya benki yametokana na kuongezeka
kwa mikopo iliyotolewa kwa wateja ambayo imeongezeka kufikia
sh 806 bil kwa Desemba 2016 toka
shilingi 754.78 bil iliyofikiwa katika
mwaka 2015.
Bi. Woiso
alisema faida kabla ya kodi imeongezeka
kwa asilimia 35 kutoka sh 17.49 bilioni mwaka 2015 hadi sh 23.66 bilioni mwaka
2016.
Alisema sehemu kubwa ya faida
imetokana na mapato yatokanayo na riba
ambayo yameongezeka kufikia sh
94.63 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 30.09, ikilinganishwa na mwaka
2015.
Kuhusu
amana, alisema zimeongezeka kwa asilimia 2% kufikia bilioni 805.94, mwishoni
mwa mwaka 2016.
Alisema,
benki hiyo imezidi kutoa huduma bora
zaidi kwa wateja wake kwa mwaka huu, huku wakiendelea kuimarisha zaidi timu yao
wafanyakazi ambao wamekuwa siri ya mafanikio hayo.
Katika hatua
nyingine, Benki hiyo ipo katika mikkati ya kuzidi kuboresha mfumo uliopo wa teknolojia ya kibenki, mfumo unaojulikana kama Flexcube 12 kutoka kampuni ya Oracle Financial Service.
Kwa upande
wa bidhaa, Bank M ilizindua bidhaa mpya katika soko inayoitwa Money inayowzesha
wateja kupaki hundi kwa ajili ya malipo moja kwa moja kutoka
ofisi zao bila kutumia njia za
kizamani ya mteja kutembelea matawi ya kibenki kuweka.
Bi. Woiso
alisema kwa mafanikio hayo, mwaka 2016 ilipata tuzo ya Benki bora katika sekta ya biashara za makampuni
Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Bank M, Jacqueline Woiso akitoa taarifa ya ripoti ya fedha ya mwisho wa mwaka 2016 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Yahaya Mbanka. (Picha na Francis Dande).
No comments:
Post a Comment