Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC),Bi.Beng’i Issa akisisitiza jambo wakati ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa Viongozi na Waratibu wa Uwezeshaji katika Kanda ya Mashariki mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro , mafunzo hayo yanafanyika Kibaha mkoani Pwani na yanaratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC). Kushoto kwake ni mwenyekiti wa bodi NEEC, Dkt.John Jingu na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Steven Kebwe.
Viongozi na Waratibu wa Uwezeshaji wa Kanda ya Mashariki wakifuatilia wakisikiliza mada wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo viongozi hao juu ya dhana ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia fursa zilizopo katika maeneo yao. Mafunzo hayo yameratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC).
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.Kebwe Steven Kebwe akisisiiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa Viongozi na Waratibu wa Uwezeshaji katika Kanda ya Mashariki mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro mafunzo hayo yanafanyika Kibaha mkoani Pwani na kuratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi NEEC, Dkt.John Jingu . wapili kushoto ni Katibu Mtendaji wa NEEC,Bi.Beng’i Issa. Kulia kwake ni Katibu Tawala- Pwani, Bw.Zuberi Semataba na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,Bi. Asumpta Mshama.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya wa Kanda ya Mashariki mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro mara baada ya kufungua mafunzo ya siku nne kwa Viongozi na Waratibu wa Uwezeshaji wa Kanda hiyo yanayofanyika Kibaha mkoani Pwani. Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo yanaratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC).
No comments:
Post a Comment