HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 18, 2017

MATOKEO MBIO ZA NYIKA TAIFA MOSHI

Washiriki wa mbio za taifa za Nyika za kilometa 10 zilizofanyika katika viwanja vya Gofu mjini Moshi.

Moshi, Kilimanjaro

MSHINDI  wa Mbio za nusu Marathoni za Kunming Plateu za nchini China, Mtanzania Emmanuel Giniki kutoka Manyara, leo amefanikiwa kushinda mbio za taifa za Nyika za kilometa 10 baada ya kushika nafasi ya kwanza akitumia muda wa dakika 28:25.


Mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya Gofu vya Moshi Club mkoani Kilimanjaro  na kushirikisha zaidi ya wanariadha 220 kutoka mikoa 11ya Tanzania, Giniki alifanikiwa kuwaacha wapinzani wake ,Basil John aliyeshika nafasi ya pili baada ya kuhitimisha mbio hizo kwa muda wa dakika 28:50 akifuatiwa na Gabriel Gerald  aliyemaliza wa tatu kwa kutumia muda wa dakika 28:54.

Washindi wengine katika mbio hizo ni ,Dickson Marwa aliyeshika nafasi ya nne akitumia muda wa dakika 29:54: ,nafasi ya tano imechukuliwa na Fabian Joseph aliyemaliza mbio akitumia muda  wa dakika 29:23 huku nafasi ya sita ikichukuliwa na Wilbert Peter aliyetumia muda dakika 29;39.

Kwa upande wa wanawake mbio za Kilometa 10, Mwanariadha Magdalena Shauri amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza akitumia muda wa dakika 33:19 akiwaacha mbali wakongwe katika mbio hizo kama Fabiliola William aliyemaliza nafasi ya saba na Banuelia Brighton aliyemaliza nafasi ya tisa.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Mwanariadha Angelina Tsere aliyemaliza mbio hizo akiwa ametumia muda wa dakika 33:42 akifuatiwa na Failuna Abdi aliyemaliza katika nafasi ya tatu huku akitumia muda wa dakika 34:25.

Mbali na mbio za Kilometa 10 pia zimefanyika mbio za Kilometa nane kwa upande wa wasichana na wavulana zikishirikisha zaidi wanariadha wenye umri chini ya miaka 19 ambapo kwa wavulana ,Mwanariadha Francis Dambel wa Manyara amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza bada ya kutumia muda wa dakika 23:30.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Yohana Elisante (23:50:01) na nafasi ya tatu ikichukuliwana Ramadhan Juma (24:09:31) huku kwa upande wa wanawake nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Cecilia Ginoka (20:24) nafasi ya pili ikichukuliwa na Asha Salum (20:58) na nafasi tatu
ikichukuliwa na Noela Remmy.

Kwa upande wa zawadi wanawake na wanaume mbio za Kilometa 10, zawadi zilitolewa kwa mshindi wa kwanza hadi wa kumi ambapo mshindi wa kwanza alijinyakulia kitita cha shilingi 400,000,mshindi wa pili tsh 300,000, mshindi wa tatu 200,000 mshindi wa nne tsh 100,000, mshindi wa tano tsh 90,000.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi ,Mgeni rasmi katika mashindano hayo Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida,Miraji Mtatiru amesema mchezo wa riadha ndio pekee unaweza kuitangaza Tanzania kitaifa na kimataifa kuliko mchezo wowote.

Taifa lina vipaji vingi kwenye cheo wa riadha licha ya kuwepo kwa changamoto ya maandalizi kwa timu za riadha kabla ya kwenda kweye mashindano huku akitoa rai kwa shirikisho la riadha Tanzania kuweka mipango yao mapema na kusihirikisha serikali iweze kutoa mchango wowote.

Ametoa ombi la kusajiliwa kwa mbio za Ikungi Marathon ambazo zimefanyika kwa kushirikisha zaidi ya wanariadha 100 wa ndani ya wilaya hiyo kwa kukimbia mbio za Kilometa  21.

No comments:

Post a Comment

Pages