NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imesaini mkataba wa
makubaliano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na Kampuni ya SunShine Group kutoka
China kwa miaka mitano kuanzia sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya
kusaini mkataba huo wa makubaliano, Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Graceana Shirima
alisema makubaliano hayo yataifanya TEA kuwa mratibu wa miradi ya kuboresha
elimu hapa nchini huku Sunshine ikifadhili na kutekeleza miradi hiyo.
Kwa mujibu wa Shirima miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa
ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mara na Mtwara ambapo miradi ya ujenzi
wa miundombinu ya shule na vifaa itatekelezwa na kampuni hiyo huku akibainisha
kwamba mikoa hiyo ndiyo yenye miradi mikubwa ya kampuni ya Sunshine.
“Miradi ya kwanza kutekelezwa kupitia makubaliano haya ni
ujenzi wa maabara mbili za sayansi katika shule za sekondari Matundasi iliyopo
Jijini Mbeya na miundombinu ya maji kwenye sekondari ya Bunda mkoani Mara
ambapo Zaidi ya sh. Milioni 210 zitatumika,” alisema Shirima.
Akiishukuru TEA, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sunshine Goup, Tony
Sun alisema kampuni yake inaona fahari kusaidia sekta ya elimu Tanzania huku
akiahidi kuendelea kuwekeza katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Alisema kampuni yake imeingia Tanzania mwaka 2012 na tayari
imetumia zaidi ya Dola 500,000 za Marekani katika elimu kwa miaka mitano ya
uwepo wao hapa Tanzania.
“Tumedhamiria kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuhakikisha
mazingira ya upatikanaji wa elimu yanakuwa rafiki na yenye kuvutia. Tunaamini TEA
watatusaidia kuzifikia shule zenye uhitaji zaidi ili watoto wetu wapate elimu
bora kwa ajili ya kujenga taifa imara,” alisema Sun.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima akifafanua jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Mkutano ukiendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Dk. Erasmus Kipesha akisaini mkataba wa makubaliano hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akisaini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, wa makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. Kushoto anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipanga, Dk. Erasmus Kipesha na Mwakili Mkazi wa Sunshin Group, Harison May.
No comments:
Post a Comment