NA MWANDISHI WETU
BENKI ya CRDB imetangaza kupata faida ya Sh. Bilioni 118.7 kwa mwaka 2016 licha ya kusemekana kwamba ni mwaka mgumu kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei alisema mafanikio hayo yanatokana na mapato ya fedha za kigeni, kukua kwa pato halisi la riba na ada, makusanyo ya tozo, na usimamizi mzuri wa gharama za uendeshaji.
“Mapato yatokanayo na riba yaliongezeka kwa asilimia 14 kufikia sh. Bilioni 568.2 kutoka sh. bilioni 497.4, wakati pato halisi la riba limeongezeka kufikia sh. bilioni 432.1 kutoka sh. bilioni 390.6 katika mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 11.
"Ada na makusanyo ya tozo yamekuwa kwa asilimia 3.8 kufikia sh. bilioni 154.5 kwa mwaka 2016 kutoka sh. bilioni 148.9 mwaka 2015,"alisema Dk. Kimei.
Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba benki hiyo inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuboresha utoaji wa huduma kupitia njia mbadala za utoaji huduma hasa kupitia simu za mkononi (SimBanking) na kupitia mtandao (Internet banking).
“Benki pia itaendelea kuelekeza nguvu zake katika kuhudumia wateja wadogo na wakati,” alisema Dkt. Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu matokeo ya kifedha ya benki hiyo kwa mwaka 2016 ambapo ilipata faida ya Sh. Bil. 118.7. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa na Katibu wa benki hiyo, John Rugambo. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu matokeo ya kifedha ya benki hiyo kwa mwaka 2016 ambapo ilipata faida ya Sh. Bil. 118.7.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu matokeo ya kifedha ya benki hiyo kwa mwaka 2016 ambapo ilipata faida ya Sh. Bil. 118.7.
No comments:
Post a Comment