Na Mwandishi Wetu
WIMBO mpya wa nyota wa muziki wa Injili nchini Miriam Lukindo Mauki 'Hakuna wa kubadili' umeanza kua gumzo kwenye mitandao ya kijamii na vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza na mtandao huu, Miriam (pichani), alisema, tangu aachie wimbo huo wiki iliyopita amekua akipokea komenti nyingi kutoka kwa mashabiki wake ambao walikua wamemmisi kwa muda mrefu kwenye gemu.
Alisema,anashukuru kuona mashabiki wake na wadau wengine wa muziki wa Injili kwa namna walivyompokea kwa nguvu na kumtaka azidi kukaza buti katika kumtumikia Mungu kupitia uimbaji.
"Nimefarijika na mapokeo ya wimbo wangu huu kwa kweli sikua mwenye matarajio kama ungeweza kua gumzo hivi kiasi sasa umeniongezea nguvu ya kuumiza kichwani nipike kazi nyingine nzuri ili kuutangaza utukufu Mungu,"alisema Miriam.
Itakumbukwa Miriam ambaye aliwahi kutamba na albamu yake ya 'Ni Asubuhi' alikua nje ya gemu kwa muda mrefu kutokana na kutingwa na majukumu ya kifamilia.
No comments:
Post a Comment