NA MWANDISHI WETU, RUVUMA
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), limetoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa kituo cha Afya katika Kata
ya Muhukuru, Kijiji cha Matama, Mkoani
Ruvuma.
Vifaa hivyo, ni mifuko 800 ya
saruji na nondo 400 zitakazosaidia kufanikiwa ujenzi wa kama njia yakuleta
maendeleo katika jamii.
Katika kufanikisha ujenzi
huo, NSSF imetoa mifuko 800 ya saruji pamoja na nondo zipatazo 400.
Akizungumza katika hafla ya
makabidhiano hayo Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji, alisema NSSF ni
shirika kubwa la hifadhi ya jamii lenye ofisi katika kila mkoa wa Tanzania na
wilaya zake.
Mpango wa ujenzi wa zahanati
hiyo umetokana na ombi la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa NSSF kuona jinsi ya
kusaidia jamii inayoshi katika Kata ya Muhukuru ambao walikuwa wanatumia kilometa 62 kufika katika zahanati ya Muhukuru.
Msaada huo wa NSSF, unalenga
kufanikisha mpango huo wa kuwapa wananchi unafuu wa kupata huduma za afya,
hivyo kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo
ya kukabidhi vifaa vya ujenzi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Oraleti
Komando aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma.
Naye Diwani wa Kata ya
Muhukuru, Manfred Mzuyu alisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwani baada
ya kukamilika, utapunguza kero wanayopata wakazi wa kijiji cha Matama.
Aidha,
diwani huyo aliongeza kuwa ujenzi huo utasimamiwa kwa ukaribu kuhakikisha
hakuna atakayehujumu ujenzi wa kituo hicho na kutoa wito kwa wengine kuiga mfano
huo wa NSSF.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Oraleti Komando, akipokea sehemu ya msaada wa mifuko 800 ya saruji na nondo 400 kutoka kwa Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji. Hafla hiyo ilifanyika mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Oraleti Komando, akimkabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na NSSF kwa Diwani wa Kata ya Muhukuru, Manfred Mzuyu. Kulia ni Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji (wa tatu kulia), Ofisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano, Amina Mmbaga (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wengini wa NSSF baada ya kukabidhi mifuko 800 ya saruji pamoja na nondo 400 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Matama, Songea.
Wakzi wa Kijiji cha Matama Kata ya Mahukuru wakiwa katika hafla hiyo.
Sehemu ya msaada wa mifuko ya saruji iliyotolewa na NSSF kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Matama, Songea mkoani Ruvuma.
No comments:
Post a Comment