Mtoto Roselyn Henry Kapinga alipata Ubatizo siku ya Jumatatu ya Pasaka ya tarehe 17/04/2017 katika kanisa la Mt. Petro Oysterbay jijini Dar es salaam na baadae kufuatiwa na sherehe fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa ndani katika Hoteli ya Wanyama Sinza jijini Dar es Salaam.
Cake maalum kwa ajili ya Ubatizo wa mtoto Roselyn Kapinga iliyoandaliwa na Aunt Agnes Makwati ikiwa tayari kwa kukatwa.
Aunt Eva (Doto) akiwa amembeba Roselyn kabla ya kuanza tukio la kukata Cake.
Mama wa Kiroho Aunt Esther Mbapila akitoa zawadi ya Roselyn kwa mama Roselyn
Cindy Makwati akimlisha cake Mama Roselyn kwa niaba ya Roselyn huku baba Roselyn akishuhudia tukio hilo.
Cindy akijiandaa kumlisha cake Aunt Agnes ambaye ni mama yake.
Babu Roselyn naye hakuwa nyuma katika kusherehekea Ubatizo wa mjukuu wake.
No comments:
Post a Comment