Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Ufundi wa Kampuni ya Tigo, Jerome Albou (katikati), akimkabidhi moja ya kompyuta Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Jangwani, Amon Mgongolwa (kushoto), ambao ni msaada wa kompyuta 10 zilizotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya matumizi ya shule, kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Dorosela Rugaiyamu na Meneja Huduma za Wateja Halima Okash. (Picha na Francis Dande).
NA NEEMA MWAMPAMBA
SHULE ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani, Dar es Salaam imepokea msaada ya Kompyuta 10 kwa ajili ya wanafunzi kuweza kujifunza Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Akizungumza wakati wa kukabidhi Kompyuta hizo Ofisa Mkuu wa Ufundi na Mawasiliano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo, Jerome Albou alisema kampuni hiyo imeamua kufanya hivyo katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wasichana Katika Tehama ili kuwezesha wanafunzi wanaopenda kitengo hicho kufanya vizuri.
Alisema Tigo imejikita katika kuchangia uwezeshwaji wa wanafunzi, hususani wasichana, ili waweze kuingia katika mtiririko wa ulimwengu katika habari na uelewa, ambapo watajifunza, na kupanua ubunifu wao na kushirikiana na wenzao kote duniani kupitia mikakati iliyo ndan ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Alisema maadhimisho ya Kimataifa ya Wasichana katika Tehama ni mkakati wa Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano ya simu (ITU) ambao unalenga kuwezesha na kuwahimiza wasichana na wanawake vijana kuzipa nafasi ajira zilizopo katika sekta ya teknolojia ya habari.
“Msaada wa kompyuta hizi upo katika mkakati wetu wa kusaidia kuwawezesha wanawake na wasichana kupitia teknolojia za habari na mawasiliano,” alisema Albou.
Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, Dorosela Rugaiyama,aliipongeza Tigo kwa mchango huo, akisema kwamba kompyuta hizo zitawafikisha mbali wanafunzi katika kusambaza stadi na uelewa wa Tehama za kisasa kwa vijana, kuwawezesha kukabiliana na changamoto za mwenendo wa mabadiliko ya habari katika jamii na duniani kwa ujumla.
Aidha alizitaka Shule za Serikali kufundisha masomo ya msingi ya kompyuta kwasababu na kuongeza kuwa hadi sasa ni asilimia 5 tu ya shule za serikali zina kompyuta hapa.
No comments:
Post a Comment