Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, akipata maelezo ya jinsi ya matumizi ya mwani na faida zake kutoka kwa mkulima wa zao hilo, Bi Mariam Pandu Kweleza katika Kijiji cha Bwejuu mjini Zanzibar. (Picha na Talib Ussi).
Bi Mariam akimwonyesha Balozi Seif mfano wa shamba la mwani na jinsi mwani unavyolimwa.
Na Talib Ussi, Zanzibar
Bi Mariam akimwonyesha Balozi Seif mfano wa shamba la mwani na jinsi mwani unavyolimwa.
Na Talib Ussi, Zanzibar
Wakulima na Wauzaji wa
mwani Zanzibar wamelalamika kodi kubwa wanazotozwa Katika ngazi tofauti za Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na bei ndogo
kwa zao hilo kwa madai kuwa haiendani na gharama za kilimo hicho.
Kilio hicho wamekitoa
katika maadhimisho ya siku ya Mwani Zanzibar ambayo imeandaliwa na tasisi ya
Milele Zanzibar Foundation mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi wakati akigagua bidhaa
zinazlishwa kutokana mwani.
Mariam Pandu Kweleza
mkulima wa mwani kutoka Kijiji cha Bwejuu, alimuambia kiongozi huyo mkuu wa
serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa kazi
wanayofanya ni ngumu na huku pato
wanalolipata si robo ya maumivu ukulima wa kilimo hicho.
“Mheshimiwa kilo 300,
kweli zitaweza kufuta jasho letu kwani kazi hii ni ngumu mnoo na sasa hivi
tuambiwa ni zao la tatu kwa kuingiza fedha za kigeni lakini wakulima bado
tunaumiaa” alilalamika bi Mariam.
Alieleza kuwa bei ya
biashara yao hiyo inapangwa na makampuni bila kuangalia kazi ngumu zinazo
fanywa na wakulima hao ambao wengi wao ni wanawake tena wajane.
Amina Khamis muuzaji wa
bidhaa zinazotokana na zao la mwani alieelza kuwa makato wanayokatwa ni makubwa
kupitia taasisi mbili tofauti kubwa ikiwemo TRA na ZRB.
Alimuomba kiongozi huyo
kuwa kuna haja ya kuziangalia upya kodi wanazokatwa ili wawe kufanyakazi yenye
manufaa kwa wakulima Pamoja na Serikali kwa ujumla.
Akizungumzi katika
ghafla ya ufunguzi wa siku ya mwani Zanzibar, Mkurugenzi Mtendaji Milele Zanzibar
Foundation Khadija Shariff alieleza kuwa tatasi yake imeamua kutoa mchango wake
kwa wakulima wa kilimo hicho kwa sababu zao hilo linalimwa na akinamama
waliowengi.
“Dira yetu ni kuona
akinamama wanainuka Kiuchumi na kuwa na mafanikio yaliobora kwa ajilia ya
kujikombo na hali ya ngumu ya maisha” alieleza Bi Khadija.
Alifahamisha kuwa
wameamua kufanya siku ya mwani maalumu kwa lengo la kulitangaza zao la mwani
ndani na nje ya Nchi ili kuvutia wawekezaji kwa ajili ya kuwapatia soko
wakulima wa zao hilo.
Akionekana kujibu
maombi ya wakulima hao, Makamu wa Pili wa Rais, alisema kuwa maombi ya wakulima
juu ukubwa wa kodi wanazotozwa wakulima hao anazichukuwa na kuahidi kuzingumza katika ngazi za Serikali ili kuona kama
waondoe au wapunguze kwa lengo la kuboresha maisha ya wakulima mwani.
“Lazima tuangalie namna
gani ya kuwafanya wakulima wetu waweze kupata manufaa” alieleza Balozi.
Alieelza kuwa wanafanya
hivyo kutokana na kufahamu Mchango mkubwa unaotokana na zao hilo licha ya
changamoto zinazowakabili wakulima.
Alieleza kuwa
watahakikisha Changamoto hizo zinafanyiwa kazi kwani tayari wamo katika mipango
ya kuazisha viwanda vya kusarifia mwani kutokana na wadau mbali mbali ndani nan
je ya nchi.
No comments:
Post a Comment