WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilayani Momba kuanzisha mradi wa ujenzi wa hospitali.
Amesema sh. milioni 900 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa
ofisi ya Halmashauri kwa sasa zianze kutumika katika kuanzisha ujenzi wa
hospitali hiyo.
Agizo hilo alilitoa jana jioni (Ijumaa, Julai 21, 2017) wakati akizungumza na wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma.
“Kwa
kuwa afya ni jambo muhimu katika utekelezaji wa kauli mbiu ya Rais Dkt. John
Magufuli ya Hapa Kazi Tu, hivyo naagiza fedha zilizotengwa kuanza ujenzi wa
ofisi zitumike katika ujenzi wa hospitali.”
Waziri
Mkuu aliwataka viongozi wa halmashauri hiyo kuongezea sh. milioni 126 katika
ujenzi huo. Fedha hizo zilitengwa kwa
ajili ya kuwafidia wamiliki wa eneo lililotengwa awali kwa ajili ya kujenga
hospitali, ambapo aliwataka watafute eneo lisilohitaji fidia.
Pia, Waziri
Mkuu aliuagiza uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) iandae ramani kwa
ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo na kuhusu suala la ujenzi wa ofisi Serikali
italishughulikia.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo baada ya Mbunge wa jimbo la Tunduma, Mheshimiwa Frank
Mwakajoka aliyeiomba kuiomba Serikali kuwajengea hospitali kwa kuwa halmashauri
hiyo haina hospitali, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi pale
wanapohitaji huduma hiyo.
Naye Mkuu
wa wilaya hiyo, Bw. Juma Irando alitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili
wilaya hiyo kuwa ni ukosefu wa hospitali ya wilaya, ukosefu wa ofisi ya Mkuu wa
Wilaya na ofisi za Halmashauri.
Pia
changamoto nyingine ni ubovu wa miundombinu ya barabara iliwemo ya
Makamba-Ikana inayotakiwa kukarabatiwa inayounganisha ukanda wa juu na chini
ili wananchi wa ukanda wa juu waweze kufika makao makuu ya wilaya.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI,
JULAI 22, 2017
No comments:
Post a Comment