Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison
Mwakyembe amewashukuru viongozi wote wa Serikali, Sekta binafsi, Taasisi za
Kidini vyombo vya habari na watanzania wote waliomfariji katika msiba wa mke
wake Bibi Linah Mwakyembe uliotokea Julai 15 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa Misa ya mazishi ya mke wake huyo
iliyofanyika jana nyumbani kwake Kyela Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa amefarijika
sana kwa upendo ulioonyeshwa na kila mtu kwa nafasi yake katika kipindi hiki
kigumu na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kila jambo.
“Mimi na wanangu tumefarijika sana kwa kuona jinsi ambavyo
Watanzania na wana Kyela mlivvyokuwa na upendo kwetu mmetupa faraja na mmetutia
nguvu na mmetuoshesha ushirikiano mkubwa katika jambo hili tunaomba mwenyezi
Mungu awabariki sana na asanteni sana”Alisema Mhe Waziri Mwakyembe.
Kwa Upande wake Mhe.Amos Makala Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati
akitoa salamu za pole kwa niaba ya wanachi wa mkoa wake amesema wananchi wa
Mbeya watamkumbuka marehemu mama Linah
Mwakyembe kwa moyo wake wa kujitolea kusaidia jamii katika mambo mbalimbali
ikiwemo kufundisha jamii kumcha Mungu pamoja na Ujasiriliamali uliosaidia
wanawake wa Kyela kujiajiri.
“Wananchi wa Mbeya tunakupa pole sana Mhe. Mwakyembe pamoja na
familia yako lakini pia tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya mama Linah
hapa duniani ambayo yameleta faida kwa jamii tunamuomba mwenyezi Mungu amlaze
mahala pema peponi amina lakini na wewe pia tunakuombea Mungu aendelee kukupa
uvumilivu na uamini kuwa hili nalo litapita”.Alisema Mhe Makala.
Marehemu Bibi Linah Mwakyembe ameagwa na kuzikwa jana nyumbani
kwake Kyela na ameacha watoto watatu.
No comments:
Post a Comment