Lengo ni kuwafikia waliowengi na huduma za kibenki kwawasio na akaunti za benki.
Dar es Salaam Tanzania, Jumatatu 14 Agosti 2017 – Ikiwa ni moja kati ya mikakati yake ya kuendelea kuboresha huduma zake kwa kutoa huduma kwa kila mtanzamia hasa kwa wale wasio na akaunti za Benki, Benki ABC Tanzania leo imezindua huduma za wakala itakayowawezesha wateja wake kupata huduma za kibenki hiyo wakiwa katika mazingira yeyote yale.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi Bi.Joyce Malai alisema Benki ABC inaendelea kuja na teknolojia mpya katika utoaji huduma ili kukidhi mahitaji ya kibenki kwa wateja wake nchini Tanzania.
Changamoto ya Kipato kidogo na kuhitajika kwa vielelezo vingi wakati wa kufungua akaunti za Benki pamoja na uhaba wa huduma za kibenki kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini yamefanya Watanzania wakose huduma za kibenki na hivyo kufanya maendeleo ya kiuchumu ya nchi kuwa finyu. Sisi Benki ABC tumejiandaa kuhakikisha kwamba huduma za uwakala za Benki yetu zinakuwa ni suluhisho kwa Watanzania kupata huduma bora za kifedha wakiwa popote bila ya kupata shida, alisema Joyce.
Aliongeza kuwa kama Benki inayokua kwa kasi hapa nchini, benki ABC inalengo kupanua huduma na uwepo wake kwenye miji mikubwa hivyo huduma za uwakala zitakuwa ni moja ya njia ya kufikia malengo hayo.
Joyce aliongeza kuwa huduma za uwakala za Benki ABC itakuwa na tija kwa Watanzania ambao hawana akaunti za Benki na pia kwa wale ambao wana akaunti lakini badala ya kupoteza muda mwingi kupanga foleni kwenye matawi yao wanaweza kupata huduma hizo kwenye wakala wa Benki hiyo popote pale. Huduma za wakala zitaanza kupatikana jijini Dar es Salaam kupitia Maxcom Afrika. Wateja wa Benki ABC watapata huduma zote za kibenki kupitia wakala wote wa Maxmalipo kwa mkoa wa Dar es Salaam kabla ya huduma hiyo kusambaa nchini kote.
Mkuu huyo wa Kitengo cha Wateja binafsi alisema wakala wa Benki ABC watatoa huduma za kibenki zikiwemo kufanya miamala mbali mbali ambazo hapo awali ziliwalazimu wateja kupanga foleni kwenye matawi ya Benki hiyo zikiwemo kuweka na kutoa fedha, kulipia ankara mbalimbali kama maji, umeme, huduma za kufungua akaunti na kupata au kubadilisha kadi ya Benki. Huduma hizi pamoja na nyinginezo zitapatikana kwa wateja wa Benki ABC kupitia Maxmalipo.
Joyce, aliwahakikishia wateja wa Benki ABC kuendelea kuwa tayari kupata huduma nyingine nyingi zenye tija na manufaa kwa ajili yao. ‘Tutaendelea kuwekeza zaidi kwenye huduma zilizo bora zaidi na kwa kuanza wateja wetu wanaweza kujidhihirishia jinsi huduma za uwakala zitakavyokuwa na tija kwao kwa kurahishisha huduma za kibenki pamoja na kuokoa gharama na muda wa kupanga foleni na kutembea umbali mrefu ili tu kupata huduma za kibenki.
Tumeungana na Maxcom Afrika Plc ambao wana mawakala wengi hapa nchini Tanzania na hivyo tunaamini tutafanikiwa sana kufikia wateja wengi na kufanikisha lengo letu, aliongeza Joyce.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Afrika Plc Jameson Kassati alisema kwa sasa mawakala wa Maxmalipo wanafanya miamala zaidi ya 700,000 kwa siku. ‘Tunajisikia fahari sana kushirikiana na Benki ABC ambayo kwa mwaka huu imeshinda tuzo ya kuwa Benki bora na inayokuwa hapa nchini Tanzania, Maxcom Afrika Plc ndio yenye wakala wengi nchini Tanzania ambapo kwa sasa kuna jumla ya wakala 16,000. Maxcom ndio ilikuwa ya kwanza kuzindua huduma za uwakala wa kibenki hapa nchini. Maxmalipo inatumia teknolojia ya utaalamu wa hali ya juu ambapo tumeweza kufanikisha kurahisisha Malipo mbali mbali kwa uharaka zaidi ikiwemo ile ya Malipo ya maji, umeme na mengineyo.
Akiongea kwenye hafla hiyo, meneja wa huduma za uwakala Benki ya ABC Mwita Robi alisema, ‘kwa hapa tulipofikia, matawi ya Benki ABC yatakuwa na umuhimu mkubwa kwani huduma zote za uwakala zitaunganisha na matawi hayo kwa ajili ya kuhakikisha viwango vya huduma zote zakibenki zinapatikana na kuzingatia taratibu zote za utoaji wa huduma za kibenki.
Huduma ya hii ya uwakala kwa mabenki inatolewa duniani kote na inatajwa kuwa moja ya njia rahisi na nyepesi ya kuwafikia wateja wengi hasa wasio na akaunti za Benki, aliongeza Mwita.
Benki ABC ambayo ni moja ya kampuni tanzu za Atlas Mara, ilishinda tuzo ya kuwa Benki bora Afrika kwa mwaka 2017 ambapo bado imeendelea kujidhatiti na kuenea zaidi hapa nchini kwa kufungua matawi mengi zaidi ambapo mwaka huu pia imejipanga kuzindua matawi mawili katika mkoa wa Dodoma na Mwanza.
Meneja wa Kitengo Binafsi Benki ya ABC Joyce Malai akiongea na waandishi wa habari wa uzinduzi wa huduma za uwakala wa Benki hiyo kwa kushirikiana na Maxcom Africa Plc.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Africa Plc Jameson Kasati akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari jana kwenye hafla ya kushirikiana na Maxcom Africa Plc kutoa huduma za kibenki.
Meneja huduma za uwakala wa Benki ABC Mwita Robi akionyesha mashine ya uwakala wa huduma za kibenki jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuzindua huduma za hiyo jana.
No comments:
Post a Comment