HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 11, 2023

RT YATANGAZA KAMATI MBALIMBALI


*Zimo Nidhamu, Rufaa, Mabadiliko ya Katiba

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limetangaza Kamati mbalimbali kwa lengo la kuboresha utendaji wa shirikisho hilo.
Kamati hizo zimetangazwa na Rais wa RT, Silas Isangi, mbele ya waandishi wa habari jijini Mwanza, leo Mei 9.
Isangi, alisema Kamati hizo zimetangazwa kwa mujibu wa katiba ya shirikisho hilo na zitadumu kwa miaka miwili, 2023-2024.


Katika kamati hizo, kumesheheni magwiji wa taaluma mbalimbali, zikiwemo sheria, mawasiliano, fedha, uchumi, masoko, madaktari, wawakilishi wa wachezaji nk.


Kwenye kamati hizo, Kamati iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ni ya mabadiliko ya katiba, kutokana na kilio cha wadau wengi, ambapo Mkutano Mkuu wa RT ulioketi Novemba mwaka jana jijini Dodoma ilikazia, ambapo Rais Isangi, amemtangaza Wakili msomi Farida Jawewa kuwa Mwenyekiti huku Katibu wake akiwa ni Katibu wa zamani wa shirikisho hilo, Wilhelm Gidabuday.


Wajumbe ni Kanali mstaafu Juma Ikangaa, Allen Allex, Charles Maguzu kutoka BMT, Katibu Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha Rogart John Steven Akhwari, Mwenyekiti Riadha Morogoro Angelius Likwembe, Boniface Tamba, wawakilishi wa wachezaji Mariam Said na Alphonce Simbu.


Kamati ya Nidhamu inaundwa na Wakili msomi Baraka Sulus ambaye ni Mwenyekiti huku Katibu ni Catherine Nyamko ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Dar es Salaam huku Wajumbe ni Gidamis Shahanga, Allen Alex na Marcelina Gwandu.


Kamati hizo kwa ujumla ni kama ifuatavyo:-

 


 

No comments:

Post a Comment

Pages