Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen
amezionya halmashauri zote mkoani Rukwa kuhakikisha wanazitumia vizuri manshine
za EFD kwa kuongeza mapato katika halmashauri zao.
Ametoa onyo hilo kwenye kikao maalum cha kujibu hoja za
ukaguzi wa hesabu za serikali kwa madiwani wa
Manispaa ya Sumbawanga katika kumalizia ziara yake maalum kwa
halmashauri zote mkoani humo kujua namna Halmashauri zilivyojipanga ili hoja
hizo zisijirudie miaka inayofuata.
Akiongea huku akionesha risiti alizozikamata katika maeneo
mbalimbali ya mauzo alisema kuwa serikali inafanya kila liwezalo katika
kuhakikisha inakusanya maopato lakini bado kuna watumishi wanatafuta namna ya
kuiskosesha serikali mapato hayo.
“katika kila sehemu za mauzo lazima mashine hizi ziwepo na
kuwepo sio mtindo huu (akionesha msururu wa risiti zilizokatwa tayari kwa
matumizi) hizi nimezikamata maeneo anajua Mkurugenzi, asubuhi watu wanagawana,
ndio mchezo uliopo, pamoja na jitihada tunazofanya bado watu wanatafuta mbinu
za kuiba, hii sio kwamba nimeleta iwe mfano, hapana, nimezikamata na mfahamu
kuwa mimi ni mtaalamu wa kukamata,”Alisema
Katika Kusisitiza suala la uwazi wa matumizi ya fedha za
halmashauri kwa waheshimiwa madiwani Mh. Zelote alitaja majukumu kadhaa ya
Mkurugenzi wa Halmashauri na kusema kuwa moja ya kazi za Mkurugenzi ni
kuhakikisha kuwa madiwani wanapata taarifa za fedha za halmashauri.
“Hapa mmezungumza na mmenionyesha kwa kiasi kikubwa kwamba
hamnazo taarifa na nikiangalia kazi moja wapo ya waheshimkwa madiwani ni
kiusimamia matumizi ya fedha za halmashauri zao sasa mtasimamiaje ikiwa hamna
taarifa,” Alisema.
Na kukumbusha kuwa Mkurugenzi ndio katibu wa kamati ya fedha
ya halmashauri lakini na kuonya kuwa kamati hiyo ibebe sura ya halmashauri na
sio sura ya kamati na kuwasisitiza kufuata taratibu nyingine za ikiwa kurudisha
mrejesho kwa wengine juu ya mipango na maazimio yaliyofikiwa.
Katika kikao hicho Mh. Zelote alimtambulisha mtaalamu wa
TEHAMA ili awaelezee waheshimiwa madiwani namna mifumo ya fedha inavyofanya
kazi ili nao wawe na uelewa mpana katika kufuatilia mapato na matumizi ya
halmashauri.
“Suala la kukusanya mapato limekuwa likiimbwa asubuhi,
mchana na usiku, kuwa tuhakikishe tunajipanga vyema kukusanya mapato ya
halmashauri kwa kupitia utaratibu uliopo, suala la kutumia hizi mashine sio la
kuhoji tena mwisho ulikuwa mwezi wa tatu ndio agizo lililopo kwa wakurugenzi
kuwa mashine hizi ziwepo na zinafanya kazi,” Alisema
Na katika kuhakikisha kuwa vitabu hivyo havipati nafasi Mh.
Zelote alitoa siku saba vitabu hivyo kurudishwa maghalani na kuongeza kuwa
watumishi wanaokiuka miiko ya kazi zao kuwajibishwa kulingana na madhara
waliyosababisha na kuwaasa kujenga uaminifu katika utumishi ndani ya
halmashauri.
“Sitaki kusikia tena kuwa kwenye mkoa wangu kuna halmashauri
inanyooshewa kidole, mmeshanyooshewa kidole mara moja sitaki kuona tena hicho
kidole,” alimalizia.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya nSumbawanga Mh.
Julieth Binyura alishanngazwa na wataalamu hao kushindwa kudhiti hoja na
hatimae wao kuwa chanzo kikuu cha kuzalisha hoja.
“Mtu kama unaitwa mtaalamu na serikali imekuamini kwanini
tena unaizalishia serikali hoja, na suala la fedha ni suala nyeti sana hivyo
linahitaji umakini wa haloi ya juu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma
inayostahili na si vinguinevyo,” Alisema.
Akifunga kikao hicho Mstahiki meya wa Manispaa ya Sumbwanga
Mh. Justin Malisawa alimuahidi Mkuu wa Mkoa kusimamia yale yote aliyoyaelekeza
na kuomba msaada wake pindi pale watakapokwama.
IMETOLEWA NA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA
No comments:
Post a Comment