WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kampuni ya SBC
Tanzania Ltd kinachotengeneza vinywaji baridi pamoja na kiwanda cha kiwanda cha
kukata na kung’arisha mawe ya asili (mabo) cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd, vilivyoko katika eneo la Iyunga Mjini
Mbeya.
Amevitembelea
viwanda hivyo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa sera ya kujenga uchumi wa
viwanda nchini, ambao ndiyo kipaumbe cha Serikali ya Awamu ya Tano. Waziri Mkuu
alivitembelea viwanda hivyo jana jioni (Jumatatu, Julai 31, 2017), akiwa katika ziara
yake ya kikazi mkoani Mbeya.
Akiwa
katika kiwanda cha Pepsi, Waziri Mkuu alikagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi
wa kiwanda hicho kwa ajili ya kuanza uzalishaji
wa vinywanji baridi kwenye chupa za plastiki, ambapo amewasihi Watanzania
kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda vya ndani.
Pia Waziri Mkuu aliishauri kampuni hiyo kuendelea kupanua
uwekezaji wake hapa nchini kwa kuwa Tanzania ina sera na mazingira mazuri ya
uwekezaji.
Kiwanda hicho kilijengwa mwaka 1999 kikiwa na wafanyakazi 75 na kwa sasa kina
wafanyakazi 190.
“Nawashauri muendelee kuwekeza Tanzania kwani mbali na utulivu wa kisiasa
pia sera na mazingira yake ya uwekezaji ni mazuri.”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi kampuni SBC Tanzania Ltd. Bw.
Atif Dar alisema kiwanda cha Mbeya ni cha pili kwa ukubwa wa mauzo ya vinywaji
baridi vinavyotengenezwa na kampuni hiyo kikitanguliwa na kiwanda cha mkoa wa
Dar es Salaam.
Alisema kwa sasa wanachukua soda zilizofungwa katika chupa za
plastiki kutoka katika kiwanda chao cha Dar es Salaam, ambapo waliamua kupanua
kiwanda hicho ili waanze kutengeneza soda zilizofungwa katika chupa za plastiki
mkoani Mbeya baada ya mahitaji kuongezeka.
Bw. Dar alisema gharama za uwekezaji huo ni dola za
Marekani milioni 3.5, ambapo mradi huo unatarajiwa kuanza rasmi Novemba 2017
ambapo mbali na kuuza katika soko la mikoa ya Nyanda za Juu Kusini pia
watasafirisha katika nchi za Zambia na Malawi.
Pia Bw. Dar alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni
10 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba katika hospitali ya Rufaa ya mkoa
wa Mbeya, ikiwa ni sehemu ya mchangamo wa kiwanda hicho katika uboreshaji wa
shughuli mbalimbali za kijamii.
Awali Waziri Mkuu
alitembelea kiwanda cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd
Waziri Mkuu alisema mbali na kukuza uchumi na kuongeza fursa za
ajira nchini, viwanda hivvyo ndivyo vitakavyowawezesha wananchi tununua bidhaa
kwa bei nafuu tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje
ya nchi.
Pia aliwataka
Watanzania wote hususani mashirika, taasisi, asasi na mamlaka za Serikali kujenga
utamaduni wa kupenda kununua na kutumia na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa
na viwanda vilivyopo hapa nchini ili
viweze kuimarika na kusaidia kutatua tatizo la ajira.
Alitoa kauli hiyo badaa ya kutembelea
kiwanda cha kukata na kung’arisha mawe ya asili (mabo) cha Marmo Granito Mines
Tanzania Ltd, kilichoko
katika eneo la Iyunga Mjini Mbeya. Kiwanda hicho kinatumia malighafi za hapa
nchini.
Waziri
Mkuu alisema mbali na kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini, viwanda
hivvyo ndivyo vitakavyowawezesha wananchi kununua bidhaa kwa bei nafuu tofauti
na ilivyo sasa kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje ya nchi.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE,
AGOSTI 1, 2017
No comments:
Post a Comment